Tazama picha mbalimbali AIC Kambarage Choir wakihudumu katika Ibada ya Jumapili ya leo, tarehe 21/12/2025 katika Kanisa la AIC Kambarage mjini Shinyanga. Ibada ilikuwa njema na yenye kuleta utukufu kwa Bwana. Katika ibada hiyo, kwaya ilipata nafasi ya kuwaaga waumini, ikiwa ni maandalizi ya safari ya kuelekea AIC Nyakato – Kahama kwa ajili ya Mkutano wa Krismasi unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 23–25/12/2025.


📣 UKUMBUSHO MUHIMU
Tunawakumbusha wapendwa wote kuendelea:
✅ Kununua tisheti na sweta rasmi za USIKU WA SHUKURANI kama sehemu ya kuunga mkono maandalizi ya tukio
✅ Kujitokeza kama wadhamini—taasisi, kampuni na watu binafsi—kwa ajili ya kufanikisha Tamasha la USIKU WA SHUKURANI linalotarajiwa kufanyika Januari 30, 2026, katika Kanisa la AIC Kambarage, Mjini Shinyanga.
Ushiriki wako ni sehemu ya baraka tele, na mchango wako unagusa maisha ya wengi.
Karibu tushirikiane kumrudishia Bwana utukufu kwa vitendo!
📞 MAWASILIANO – MANUNUZI YA TISHETI & UDHAMINI
📱 +255 685 788 063 – AICT Kambarage Choir
📍 Wauzaji Shinyanga:
• Majengo & Mjini: Leonadia – +255 614 028 803
• Kambarage & Ndala: Abel – +255 628 495 081













Post a Comment