Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro, ametangaza kufariki kwa mmoja kati ya watu wanne waliookolewa katika ajali ya kufukiwa na mgodi katika machimbo ya Nyandolwa wilayani humo, ambapo watu 25 walifukiwa Agosti 11 mwaka huu.
Amesema marehemu, Emmanuel Kija, alikolewa akiwa hai lakini hali yake ikiwa mbaya, na licha ya jitihada za madaktari kumuwekea mashine ya kupumua, alifariki dunia.
Mtatiro amesema majeruhi mwingine, Fulano Peter, amepelekwa Bugando Jijini Mwanza kutokana na hali mbaya, huku wengine wawili wakiendelea kutibiwa Hospitali ya Rufani Shinyanga.
Naibu Waziri wa Madini, Steven Kiruswa, ametaka ukarabati wa maduara mgodini ufanyike kwa mpangilio na tahadhari, ili kuepusha mitikisiko inayoweza kusababisha udongo kuporomoka.
Ameomba wananchi kusubiri kwa subira na kuendelea kumuomba Mungu ili watu 21 waliobaki chini ya kifusi waweze kuokolewa wakiwa hai.
Post a Comment