" MANISPAA YA SHINYANGA YAANZA RASMI SAFARI MASHINDANO YA SHIMISEMITA MKOANI TANGA

MANISPAA YA SHINYANGA YAANZA RASMI SAFARI MASHINDANO YA SHIMISEMITA MKOANI TANGA

MKURUGENZI WA MANISPAAYA SHINYANGA MWL. ALEXIUS KAGUNZE WA PILI KUTOKA KUSHOTO MSTARI WA MBELE AKIMKABIDHI BENDERA YA MANISPAA YA SHINYANGA, MKUU WA MSAFARA WA WANAMICHEZO WA MANISPAA YA SHINYANGA AMBAYE NI AFISA UTUMISHI HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA NDG.  JACOBO MWAKISU 

NA. ELIAS GAMAYA- SHINYANGA.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Mwl. Alexius Kagunze, amewatakia kila la heri wanamichezo wa Manispaa ya Shinyanga wanaokwenda kushiriki mashindano ya SHIMISEMITA mkoani Tanga, huku akiwasisitiza uwajibikaji, nidhamu na kujituma kwa kila mmoja wao ili kufanikisha ushindi.

Akizungumza leo, Agosti 15, 2025, wakati wa kuagana nao kabla ya kuanza safari, Mwl. Kagunze amesema Halmashauri inaimani kubwa sana na wanamichezo hao kufanya vizuri ili kuhakikisha timu hiyo inapata tuzo.

“Nendeni mkaiwakilishe vyema bendera ya Manispaa ya Shinyanga tunamatumaini  kubwa sana na nanyi. Kila mmoja wetu twendeni tukashirikiane, tujitume na kupigania ushindi. Ubora tunao, nia tunayo, na shauku ipo sasa ni wakati wa utekelezaji.” amesema Mwl. Kagunze.

Mashindano ya SHIMISEMITA yameanza Agosti 15 na yanatarajiwa kumalizika Agosti 29, 2025, yakihusisha timu kutoka halmashauri mbalimbali nchini.

  

Post a Comment

Previous Post Next Post