MSIMAMIZI MSAIDIZI WA UCHAGUZI WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI, NDG. SAIMON SHOO (kushoto) AKIMKABIDHI FOMU ZA UTEUZI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI NDG. GERALD MSHANDETE LUBASHA KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI (CUF) (kulia)
NA. ELIAS GAMAYA- SHINYANGA
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Shinyanga Mjini,
Ndg. Saimon Shao leo agosti 19, 2025 amekabidhi fomu za uteuzi mgombea wa
nafasi ya Ubunge ndg. Gerald Mshandete Lubasha jimbo la Shinyanga Mjini
Kupitia CHAMA CHA WANANCHI (CUF)
Ndg. Lubasha anakuwa mgombea wa nne kuchukua fomu za
Uteuzi kugombea ubunge kwa jimbo la Shinyanga Mjini ambapo jumla ya vyama
11 vilivyosajiliwa kwa jimbo hili vinatarajiwa kushiriki katika mchakato huo.
Zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi ya Ubunge
umeanza rasmi hapo jana Agosti 14, 2025 ambapo linatarajiwa kutamatika Agosti
27, 2025 ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, utakaofanyika
Oktoba 29, 2025.
Post a Comment