" MUSABE YAPONGEZWA KWA KUENDELEA KUFAHAULISHA WANAFUNZI

MUSABE YAPONGEZWA KWA KUENDELEA KUFAHAULISHA WANAFUNZI

Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaShule za Musabe ya Awali na Msingi zimepongezwa kwa kuweza kutunza kumbukumbu ya kufaulisha wanafunzi wote darasani kwa kiwango cha gredi A katika mitihani ya kitaifa tangia kuanza kwake mwaka 2017.Akizungumza katika mahafali ya darasa la saba na shule ya Awali Jijini Mwanza wadau hao wamesema kuwa jitihada hizo ni kitu cha kupongezwa kwani inaonesha namna wanafunzi hao wanavyofanya vizuri kitaaluma katika shule hiyo.Afisa Elimu ya Msingi na Awali Jijini Mwanza,   Mussa Lambwe aliipongeza Shule  hiyo kwa kuendeleza matokeo ya gredi A kwa wanafunzi wake wanaomaliza darasa la saba na wanaohitimu shule ya awali.Aliwapongeza vilevile kwa kuwa na ufundishaji wa lugha za kigeni kama vile kichina, kingereza na Kifaransa na masomo ya komputa kuanzia skuli ya awali kwani hatua hiyo inawafanya wanafunzi kuwa na uelewa mkubwa wa lugha hizo.Aidha Afisa Elimu huyo alisema serikali inathamini michango inayofanywa na wadau wa maendeleo katika kufanikisha utoaji wa elimu kwenye jamii hivyo kufanya taifa kupiga vita ujinga.Mkurugenzi Mtendaji wa shule hiyo, Daniel Damian alisema kuwa kuwapa motisha walimu na kuwepo kwa mazingira mazuri ya kujifunzia kuwa ni sababu inayopelekea kuwepo kwa ufaulu huo katika skuli hiyo iliyopo Jijini Mwanza."Tuna hakikisha kuwa wanafunzi hawapati changamoto za kuwafanya washindwe kutilia maanani masomo yao" alisema Damian.Mzazi wa  mhitimu wa darasa la saba Japheth Kyaruzi alisema anafurahia matokeo ambayo shule hiyo imekuwa ikipata hivyo ana Imani kuwa mwanaye atakuwa miongoni mwa atafanya vizuri katika Mtihani wa Mwezi9 Mwaka huu Uku Mtoto Caleni Japheth akiwa na Mtoto ya Kuwa Mfanyabiashara Kama Bhakhersal

 


Post a Comment

Previous Post Next Post