" TRA YAWAHIMIZA WAFANYABIASHARA BUKOBA KUTAMBUA UMUHIMU WA MABADILIKO YA SHERIA ZA KODI NA KUTEKELEZA WAJIBU WAO WA KULIPA KODI KWA HIARI

TRA YAWAHIMIZA WAFANYABIASHARA BUKOBA KUTAMBUA UMUHIMU WA MABADILIKO YA SHERIA ZA KODI NA KUTEKELEZA WAJIBU WAO WA KULIPA KODI KWA HIARI

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media - BukobaMAMLAKA ya mapato Tanzania (TRA)imefanikiwa kuwakusanya  walipakodi wa wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera na kuwapa elimu juu ya mabadiliko ya sheria za kodi katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2025/2026  huku ikiwahimiza kutambua kuwa mabadiliko ya sheria mbali mbali ambayo yamesomwa hivi karibuni Bungeni mnamo  mwezi Juni mwaka huu  yana umuhimu mkubwa kwao.Elimu hiyo kwa wadau hao na wafanyabiashara imefanyika Agosti 19, 2025 katika ukumbi wa BCD Hotel uliyopo Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera  ambapo Wafanyabiashara hao wamezidi kuchota maarifa hayo kutoka mamlaka hiyo.akizungumza baada ya mafunzo hayo Afisa msimamizi wa kodi (TRA) Abdalla Seif Abdalla amesema kuwa kutokana mabadiliko mbali mbali ya sheria za kodi yaliyojitokeza ikiwemo kodi ya mapato, ushauri wa bidhaa na mengineyo ni vyema Wafanyabiashara waelewe kuwa mabadiliko hayo yametolewa na wajitahidi kuyajua kwa undani."Sisi kama TRA tumechukua jitihada katika maeneo mbali mbali kutoa elimu  hivyo nasisitiza kuhakikisha wafanya biashara mnajenga utamadani wa kuitikia wito inapotokea tangazo au matangazo ya kuwahitaji ili mfanikishe masuala mbali mbali ya ulipaji wa Kodi kwa usahihi.Kwa upande wake afisa msimamizi wa kodi Mecy Macha amesema kuwa Watanzania wanatakiwa wajue kwamba serikali inasikia na inatekeleza kile kinachotolewa kama maoni na mapendekezo na kisha kurekebisha pale makosa yaliyofanyika hivyo waendelee kuamini na kuyafanyia kazi mapendekezo yanapotolewa.Bi Macha amewataka wadau hao na wafanyabiashara kutoa taarifa za kuwafichua wanaokwepa kulipa kodi kwani wanadidimiza maendeleo.Hata hivyo afisa elimu na mahusiano TRA Kagera Rwekaza Rwegoshora amewashukuru  wafanyabiashara hao pamoja na wadau mbali kujitokeza kwa wingi kuvuna maarifa hayo huku akiwapongeza waliolipa  kodi kwa hiari kwa mwaka ulioisha na kuwakumbusha kuendelea kufanya hivyo  ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.


 

Post a Comment

Previous Post Next Post