Na: Belnardo Costantine, Misalaba Media Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dkt. Samia Suluhu Hassan.amezindua rasmi Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki kinachotambulika kwa jina maarufu "EACLC" kilichopo jijini Dar es Salaam wilaya ya ubungo .Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 1 Agosti, 2025.Aidha Mradi huu ulianza kutekelezwa mnamo Mei 2023 na umetajwa kugharimu Shilingi bilioni 282.7 hadi kufikia hatua ya kukamilika kwake.Hatahivyo EACLC inatarajiwa kutoa zaidi ya ajira 15,000 za moja kwa moja, huku ajira zisizo rasmi zikiwa zaidi ya 5,000. Hii inatajwa kuwa ni hatua kubwa katika kukuza ajira, hasa kwa vijana na wanawake.Sambamba na hilo kituo hiki kinatajwa kuunga mkono uwekezaji wa ndani na kimataifa, huku kikipa mkono viwanda vya uzalishaji wa ndani na kuongeza thamani kwa bidhaa za Tanzania.

Post a Comment