Umoja wa Afrika (AU) umeunga mkono kampeni ya kusitisha matumizi ya Ramani ya dunia ya Mercator iliyochorwa katika karne ya 16 ambayo umekuwa ikitumiwa na Serikali pamoja na Mashirika ya Kimataifa na badala yake kuhimiza matumizi ya ramani inayoonesha uhalisi wa ukubwa wa bara la Afrika.
Ramani hiyo iliyochorwa na mbunifu na mchora ramani Gerardus Mercator kwa Uabiri, makadirio hayo yanapotosha ukubwa wa bara na kupanua maeneo karibu na ncha kama vile Amerika Kaskazini na Greenland huku ikipunguza Afrika na Amerika Kusini ambapo Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Selma Malika Haddadi amesema “ Inaweza kuonekana ni ramani tu kawaida lakini kiuhalisia Afrika haipo hivyo.”
Haddad ameliambia shirika la habari la reuters kuwa ramani ya Mercator imekuza fikra potofu kwamba Afrika ilikuwa pembezon na bara hilo halina umuhimu licha ya kuwa bara la pili kwa ukubwa duniani kwa eneo, lenye zaidi ya watu bilioni moja na Umoja wa Afrika (AU) una nchi wanachama 55.
Kampeni ya ukosoaji wa ramani ya Mercator sio jambo jipya kumekuwa na mashirika kama vile ‘Afrika No Filter’ na Speak up Afrika’ yamekuwa mstari wa mbele kurekebisha ramani ya dunia kwa kumshisha kampeni ya “sahihisha Ramani” iliyoanzishwa mwaka 2018 iliyokuwa ikilenga kuyahamasisha mashirika ya kimataifa kutumia ramani sahihi ya dunia ya “Equal Projection” inayoonesha ukuwa sahihi wa bara la Afrika.
Haddadi amesema Umoja wa Afrika (AU) imeidhinisha kampeni hii kwa sababu inalenga “kurejesha nafasi sahihi ya Afrika katika majukwaa ya kimataifa” sambamba na wito unaoongezeka wa fidia kutokana na ukoloni na utumwa na Ameongeza kuwa Umoja wa Afrika utahamasisha matumizi mapana ya ramani hiyo na kujadiliana na nchi wanachama kuhusu hatua za pamoja za utekelezaji.
Post a Comment