Waandishi wa habari wa Mkoa wa Tabora wamepewa mafunzo ya ulinzi na usalama hasa wakati wa utekelezaji wa majukumu yao hasa katika kipindi muhimu tunachoelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29 mwaka huu.
Akifungua mafunzo hayo ya siku moja ambayo yamefanyika katika Hoteli ya Frank Man ambayo yamehudhuriwa na waandishi wa habari 22 mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari Mkoa wa Tabora Juma Kapipi amesema kuwa mafunzo hayo ni muhimu na yamekuja wakati sahihi na kuwataka washiriki wazingatie na kuyafanyia kazi kwa manufaa yao na jamii kwa ujumla.
"Nina waomba waandishi wenzangu tuzingatie haya mafunzo tutakayofundishwa leo na mkufunzi wetu kwani haya ni mafunzo muhimu kwetu na yamekuja kwa wakati sahihi ambapo tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu octoba mwaka huu"alisema Kapipi.
Mwenzeshaji wa mafunzo hayo Hadija Omary Mazezele ambaye ni mwandishi wa habari wakati anawasilisha mada ya ulinzi na usalama kwa waandishi wa habari hao alisema waandishi wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotekeleza majukumu yao ya kazi kwa kujilinda wakati wote kwani ulinzi na usalama huanzia kwa mwandishi mwenyewe.
Aidha amewataka waandishi wa habari kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao akisema ndio vitakuwa nguzo kuu ya kulindana na kusaidiana hasa zinapotokea changamoto za kiusalama kwa waandishi zinazoweza kuathiri utendaji kazi wao
Kwa upande wake Mshiriki wa semina hiyo Olivina Benjamini amesema mafunzo hayo yamemuwezesha kutambua baadhi ya vitu ambavyo vimemfumbua macho hasa kuelekea uchaguzi mkuu ili kuhakikisha anakuwa salama na kujua mipaka yake kama mwandishi itakayolinda usalama wake
Naye Mk Magesa amesema mafunzo hayo yamewafungua na kuwapa mwanga mkubwa katika kujikinga wao wenyenwe na vifaa vyao pamoja muonekano wao ambao utaweza kuwapa utambulisho chanya katika jamii na kijepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Mafunzo hayo yanatolewa chini ya mradi wa Empowering Journalists for Informed Community (Kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili jamii iweze kupata taarifa) unaotekelezwa na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kwa kushirikiana na (IMS) ambapo miongoni mwa maeneo ya mradi huo ni kuhusu masuala la ulinzi na usalama wa mwandishi wa Habari, usalana wa mwandishi wa Habari Mtandanoni na Digital Safety Training and Tackling Online Gender-Based Violence for women journalists
Post a Comment