Na: Mwandishi Wetu, DAR
Wanafunzi, wazazi na walezi wamesisitizwa kuzitumia vyema siku kumi zilizobaki kukamilisha maombi ya mikopo na Samia Scholarship kwa mwaka 2025/2026, kabla dirisha la uombaji mikopo ya elimu ya juu halijafungwa Agosti 31, 2025.
Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Agosti 21, 2025, imesisitiza kuwa dirisha la uombaji mikopo lilifunguliwa rasmi Juni 15, 2025 na litafungwa rasmi Agosti 31, 2025 ambapo hakutakiwa na muda wa nyongeza baada ya dirisha la uombaji mikopo kufungwa rasmi.
Hivyo basi, wanafunzi wenye sifa ambao hawajakamilisha maombi yao wamehimizwa kukamilisha maombi yao ili waweze kunufaika na mikopo ya elimu ili kutimiza azma yao ya kupata elimu ya kati na ya juu.
Ikumbukwe kuwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026, HESLB imeidhinishiwa shilingi bilioni 916.7 ili ziweze kugharamia wanafunzi wapatao 252,773.
Post a Comment