Na Mwandishi wetu, Misalaba Media Hekaheka Uchaguzi Mkuu October 2025 zinaendelea ambapo wagombea Mbalimbali Wanaendelea kujitokeza kuchukua Form za Udiwan akiwemo Kada wa chama cha Mapinduzi( Ccm)Eng Mfinanga ambaye juzi amechukua Fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani katika kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza kupitia tiketi ya Chama hichoZoezi la Uchukuaji fomu hiyo limefanyika katika Ofisi za Mtendaji Kata ya Buhongwa ambapo Mfinanga amekabidhiwa Fomu na Ambaye Ni katibu wa Wilaya ya Nyamagana Deogratius Nakey akisindikizwa na Wanachama Pamoja na wananchi .Akizungumza Baada ya kuchukua fomu Mfinanga ametoa Shukrani zake kwa Ccm kwa kumpa Ridhaa ya kupeperusha Bendera ya Chama hicho katika nafasi ya Udiwani Kata ya Buhongwa “ sintakuwa na Mengi sana zaidi ya yote ninawashukuru sana Mliojitoa na kunisindikiza kukamilisha zoezi la Uchukuaji wa Fomu nikishukuru Pia chama changu kwa Kuniteua kupeperusha Bendera na kwa sababu tutarudi ntakuja kuwaeleza kwanini? Nimetuma kugombea Udiwani Kata hii.

Post a Comment