Wapanda baiskeli wanaojihusisha na shughuli za kusafirisha abiria katika eneo la Nguzo Nane, Manispaa ya Shinyanga, wamepatiwa elimu ya usalama barabarani ili kuwaepusha na ajali zinazoweza kujitokeza wakati wa shughuli zao za kila siku.
Elimu hiyo imetolewa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, ambaye amewasisitiza kutumia upande sahihi wa barabara wanapokuwa safarini.
Katika mafunzo hayo, Sajenti Ndimila pia amebaini kasoro mbalimbali kwenye baiskeli zinazotumika kwa shughuli hizo, ikiwemo kukosekana kwa kengele, breki imara na taa, na kueleza kuwa mapungufu hayo yakiachwa bila kurekebishwa yanaweza kusababisha ajali.
Wapanda baiskeli hao wameelekezwa kuhakikisha wanarekebisha mapungufu hayo mapema ili kujihakikishia usalama wao pamoja na abiria wawapo barabarani.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment