Na Lydia Ezra Lugakila Mbeya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe, Beno Malisa amewaomba wananchi mkoani Mbeya kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwasili mkoani humo mnamo septemba 4, 2025.Mhe, Malisa ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi mkoani Mbeya waliojitokeza kwenye matembezi ya hisani kwa lengo la kujiweka tayari kwa mapokezi ya Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta Samia Suluhu Hassan anayetarajiwa kuwasili mkoani humo kuzungumza na wananchi.Mkuu huyo wa mkoa pia ametumia fursa hiyo kuwawata Wananchi mkoani humo kujitokeza kwa wingi katika kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru Oktoba 14, 2025 kitakachoambatana na wiki ya vijana kitaifa na kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere Ameongeza kuwa Sherehe hizo za kilele zitafanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya zikiwa zimebeba kauli mbiu isemayo " jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu"Matembezi hayo yaliyoandaliwa na Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya Mbeya Solomon Itunda yamehusisha makundi mbali mbali yakiwemo vikundi vya mbio za pole ya mkoani Mbeya, vijana wajasiliamali, Mama na Baba lishe, watumishi wa Serikali na wanafunzi wa vyuo vya kati na vyuo vikuu.Baadhi ya wananchi walioshiriki matembezi wameeleza sababu ya kuhamasika kushiriki ikiwa ni pamoja na kazi kubwa zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita katika kutimiza malengo kwa wananchi wake hususani kwenye mkoa wao wa Mbeya.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment