Na Elisha Petro, Misalaba Media
Mgombea udiwani wa Kata ya Ndala, Mheshimiwa Zamda Shaban Mwembea, amechukua fomu ya uteuzi, tarehe 19 Agosti 2025, tayari kujiandaa kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Baada ya kuchukua fomu hiyo, Mhe. Mwembea ameahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa kata hiyo kwa moyo wa dhati na bila kuchoka, huku akisisitiza lengo lake la kuchochea maendeleo kupitia shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi.
Mhe. Mwembea ameeleza kuwa dhana yake kuu ya maendeleo ni kuhakikisha Kata ya Ndala inapata huduma bora za afya, elimu, miundombinu na fursa za kiuchumi kwa vijana na wanawake.
Amesema atashirikiana na wananchi na wadau mbalimbali kutekeleza miradi ya maendeleo itakayoboresha maisha ya kila mwanakitala.
Aidha, amesisitiza kuwa yote atakayofanya yataendana na Ilani na maelekezo ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiahidi kushirikiana kwa karibu na chama chake na wananchi kuhakikisha kila hatua inachangia maendeleo ya kata.
Pia, amewaomba wananchi kuendelea kumpa ushirikiano wakati atakaporejesha fomu yake na katika kipindi chote cha uchaguzi mkuu, akiahidi kushirikiana nao kwa karibu ili kuhakikisha maendeleo ya kata ya Ndala yanaendelea na kila mwananchi anaona matokeo chanya ya maendeleo.
Post a Comment