" DKT. TULIA ACKSON AENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO WA CCM NA WANANCHI WA MAKETE

DKT. TULIA ACKSON AENDELEA KUIMARISHA UHUSIANO WA CCM NA WANANCHI WA MAKETE


Na Lydia Lugakila, Misalaba Media

Uzinduzi wa Kampeni za Ubunge Jimbo la Makete

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Dkt. Tulia Ackson,  ametangaza rasmi uzinduzi wa kampeni za Ubunge wa Jimbo la Makete kupitia chama hicho. 

Uzinduzi huo umefanyika Septemba 14, 2025 katika viwanja vya Mabehewani, kata ya Iwawa, Makete mkoani Njombe, na umeambatana na kumnadi mgombea ubunge wa jimbo hilo,  Festo Sanga, pamoja na madiwani wa Jimbo la Makete.

Katika hotuba yake, Dkt. Tulia amewasisitizia wananchi wa Makete na Tanzania kwa ujumla kuwaendeleza kuamini CCM, akiwataka wapige kura nyingi za ndiyo katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025. Amesisitiza kwamba CCM ndicho chama chenye ilani bora inayobeba matumaini ya wananchi. 

Uzinduzi huu unaleta matumaini miongoni mwa wana CCM na kuimarisha uhusiano kati ya chama na wananchi katika kuelekea uchaguzi huo muhimu.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post