" ASKOFU LYIMO ATEULIWA KUWA ASKOFU WA KWANZA WA JIMBO JIPYA LA BARIADI

ASKOFU LYIMO ATEULIWA KUWA ASKOFU WA KWANZA WA JIMBO JIPYA LA BARIADI



 Baba Mtakatifu Leo XIV, leo tarehe 08.01.2026, amemteua aliyekuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu Arusha Mhashamu Prosper Baltazar Lyimo, kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo jipya la Bariadi.

Askofu Lyimo alizaliwa mnamo Agosti 20, mwaka 1964 ambapo baada ya masomo ya majiundo yake ya kipadre alipewa Daraja takatifu la Upadre mnamo Julai 04 mwaka 1997 Jimboni Arusha.
Askofu Lyimo ambaye ana shahada ya uzamivu (PhD) katika sheria za Kanisa, alikuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Arusha tangu mwaka 2015.
Tarehe ya kusimikwa rasmi kwa Askofu Lyimo kuwa Askofu wa kwanza na mwanzilishi wa Jimbo jipya la Bariadi, itatangazwa hapo baadaye.

TAARIFA RASMI 🚨: Baba Mtakatifu Leo XIV amemteua Askofu Msaidizi Prosper Baltazar Lyimo aliyeukwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Arusha, kuwa Askofu wa Kwanza na Mwanzilishi wa Jimbo jipya la Bariadi.

Chanzo - Radio Faraja

Post a Comment

Previous Post Next Post