Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya mjini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Patrick Mwalunenge, amesema kuwa endapo atapata nafasi ya kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha kuwa watoa huduma, hususan katika sekta ya afya, wanatoa huduma bora bila kuwanyanyasa wananchi. Mwalunenge ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika katika eneo la Kabwe, Mbeya mjini.Amesema kuwa atakuwa na ushirikiano wa karibu na watoa huduma wa afya na atawachukulia hatua kali wale ambao hawajali wagonjwa. "Nitalala nao mbele kwa mbele," alisema, akiongeza kwamba ameona ahadi muhimu za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha huduma za afya ikiwemo ujenzi wa hospitali mpya na upatikanaji wa matibabu bure kwa wananchi wasio na uwezo" alieleza mgombea ubunge huyo.Mwalunenge pia ametangaza kuwa wazee kuanzia miaka 60 hawatabughudhiwa huku watoto chini ya miaka mitano wakitarajiwa kutibiwa bure.Mgombea huyo amesema atabadili Jiji la Mbeya ili liweze kufanana na miji mikubwa kama Pretoria au Johannesburg, huku kuahidi kufanya kazi kwa bidii kuboresha miundombinu ya barabara.Aidha, amesema atatatua migogoro ya ardhi na kuanzisha meza maalum za biashara kwa akina mama ili waweze kufanya biashara zao kwa urahisi. Mwalunenge pia amesisitiza umuhimu wa kuwa na soko kubwa la kimataifa la biashara ili kariakoo ndogo ihamie Mbeya.Katika kutimiza azma yake, Mwalunenge amewaomba wananchi kumchagua kwa kura nyingi ili kufanya mabadiliko makubwa katika Mkoa wa Mbeya na kuhakikisha kuwa wanaishi katika mazingira bora. "Ni lazima katika kipindi changu cha ubunge, tutajenga kumbi za mikutano mikubwa itakayofanyika Mbeya," alihitimisha Mwalunenge.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA


Post a Comment