Na Lydia Lugakila , Misalaba Media -MbeyaSpika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Tulia Ackson, amesema kuwa hakuna chama chochote cha siasa nchini kinachoweza kutatua changamoto za wananchi kwa dhamira ya dhati zaidi ya CCM. Dkt. Tulia ametoa kauli hiyo Septemba15, 2025 wakati wa ufunguzi wa kampeni za Ubunge wa Jimbo la Kyela mkoani Mbeya wakati akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo Baraka Mwamengo katika viwanja vya Kyecu, kata ya Ipinda.Amesema kuwa wananchi hawapaswi kufanya makosa katika kuchagua vongozi watakaowavusha salama na kwamba itapofika Oktoba 29, 2025 wahakikishe wanampigia kura za kishindo Dkt. Samia Suluhu Hassan katika nafasi ya Urais sambamba na Wabunge na Madiwani wa chama hicho."Ndugu zangu wana Kyela, leo nataka niwahakikishie kwamba hakuna mtu wala chama chochote zaidi ya CCM kinachoweza kutekeleza matamanio na matarajio yenu kwakuwa chama hiki ndicho chenye Ilani bora inayotekelezeka na mtekelezaji wake mkuu ni Dkt. Samia Suluhu Hassan" amesisitiza Dkt. Tulia








Post a Comment