Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Mbeya
Mgombea ubunge Jimbo la Uyole Dkt. Tulia Ackson amefika kata ya Isanga na kueleza mazuri ambayo ameyafanya mgombea udiwani wa kata Isanga Dormohamed Issa kwa kipindi cha miaka mitano na kuwaomba wana Isanga kumchagua tena kuwa Diwani kwa miaka mitano ili kukamilisha alipoishia na kuonyesha mabadiliko mapya ndani ya kata hiyo.
Dokta Tulia ametoa kauli hiyo septemba 10,2025 wakati wa ufunguzi wa kampeini kata ya Isanga alipofika kuwasalimia wananchi hao hasa lengo likiwa ni kuwaeleza mambo mazuri yaliyofanyika katika kipindi cha miaka mitano chini ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Dokta Tulia amesema kuwa kila mmoja amejionea kazi kubwa iliyofanywa na Mhe Issa Dormohamed huku akiwaomba wananchi hao kumpigia kura za kutosha Ifikapo Oktoba 29,2025 pamoja na wagombea wote wa CCM ikiwa ni pamoja na kumuheshimisha kwa kura za kishindo na za heshima mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dokta. Samia Suluhu Hassan pamoja na mgombea ubunge Jimbo la Mbeya mjini Patrick Mwalunenge.
Amesema kuwa katika upande wa miundombinu tayari Barabara zimejengwa kwa viwango katika kata ya Isanga kwa nguvu na juhudi kubwa za Bwn Issa ambapo eneo la Afya nalo limeboreshwa, Ofisi ya kata imejengwa ikiwa ni hatua za kujiongeza kwake huku shule za msingi na sekondari zikiboreshwa na madawati ya kutosha kupatikana ili kuruhusu watoto kutokukaa chni.
Dokta Tulia amesema yale yaliyosalia watayamalizia kwa awamu ijayo huku akiwaomba wananchi wa kata ya Isanga kuwachagua viongozi wa chama hicho kwa maendeleo bora.
Adha amepongeza nguvu na umahili wa mgombea udiwani huyo kutokana hatua iliyofanyika katika kipindi cha miaka mitano ambapo upande wa shule za sekondari na msingi hakuna mtoto anayekaa chini kwani madawati yametolewa ya kutosha.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment