" DORMOHAMED ISSA AZIDI KUVUTIA AELEZA JINSI DOKTA TULIA ALIVYOMNOA KATIKA SIASA AMTAJA KAMA MWALIMU WAKE

DORMOHAMED ISSA AZIDI KUVUTIA AELEZA JINSI DOKTA TULIA ALIVYOMNOA KATIKA SIASA AMTAJA KAMA MWALIMU WAKE

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media 

Mbeya

Mgombea wa udiwani kata ya Isanga kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mhe, Dormohamed Issa amemwagia sifa Mhe Dokta Tulia Ackson na kumtaja kuhusika pakubwa katika kumuinua kisiasa hadi kuvutia katika nafasi yake.

Mhe Issa ametoa kauli hiyo katika uzinduzi wa kampeini za chama cha mapinduzi (CCM) zilizofanyika kata ya Isanga Mbeya mjini.

Mhe, Issa amesema kuwa bila Dkt. Tulia yeye asingeweza kufanya chochote kwani amekuwa mwalimu wake katika upande wa siasa na maisha na kuwa amekuwa msaada mkubwa katika kuleta ushawishi wa maendeleo jambo ambalo limemvusha Diwani huyo na kuonekana kuwavutia watu wengi.

"Jambo likinizidi sitoacha kugonga hodi kwako Dokta Tulia amekuwa msaada mkubwa kwangu pia wana Uyole hamjakosea Uyole inakwenda kutajirika kwa haraka kwani mna mtu anayependa maendeleo na watu wake alisema Mhe, Issa.

Amemtaja Dokta,Tulia kama mtu mwenye subira, mvumilivu na kuwa ushawishi wake kwenye maendeleo amemfanya diwani huyo kuwa mahiri katika siasa  kwani amejifunza kutoka  kwake.

Amewaomba wana Isanga kukiheshimisha chama cha mapinduzi ifikapo Oktoba 29 mwaka huu kwa kura nyingi za mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dokta.Samia Suluhu Hassan, pamoja na mgombea ubunge Jimbo la Mbeya mjini Patrick Mwalunenge ambaye anatarajia kuipeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya ubunge na kuwaomba wana Isanga kumpa kura za kutosha.

Issa amesema aliahidi Barabara za kiwango cha lami, ujenzi wa zahanati,ujenzi wa Ofisi ya kata ambapo ametekeleza pakubwa huku miradi mingine ikiwa imefikia hatua ya kuelekea kuanza kutumika.

Ameongeza kuwa fedha nyingi zimetumika kukarabati madarasa katika shule mbali mbali za msingi na sekondari pamoja na miundombinu ya vyoo huku kero za barabara zikiendelea kufanyiwa kazi lengo likiwa ni kukiheshimisha chama cha mapinduzi na kuwajali wananchi wake .

Aidha mgombea huyo amewaomba wananchi hao kumpigia kura za kutosha Rais Samia kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ikiwemo kuwezesha katika miradi mikubwa.

Amewasisitiza wana Uyole kumpa Dokta Tulia kura za heshima kwani ameletea heshima kubwa kutokana na uongozi wake imara kwani amefanya kazi kubwa ikiwemo kuwajali watu wa rika zote.

"Wananchi nawaomba tuwape kura za kutosha madiwani wa CCM kwani wamefanikisha miradi mikubwa hivyo tuendelee kuwasemea madiwani wetu" alisema Issa.

Aidha amemshukuru Dokta Tulia kwa heshima aliyoinesha kwa wana Isanga kwa kufika na kuwasalimia huku wakiahidi kuwa mapenzi yao kwake hayatakatika kamwe.

Kwa upande wake  ya mhe Lucas Mwampiki amesema muda wa kubahatisha umeisha kwani matokeo ya kuiamini CCM yameonekana hivyo shukrani zao kwa Chama Cha Mapinduzi ni kuwapa kura za kutosha.

Hata hivyo baadhi ya viongozi waliopanda jukwaa hilo walimtaja ndg Issa kama mtu mpambanaji anayesikiliza watu bila kuwabagua na mwenye kujua wajibu wake huku wakimpongeza kwa namna ambavyo amekuwa kiongozi wa mfano katika kata hiyo katika kipindi cha miaka mitano kwani Isanga imebadilika kwa kasi ya haraka.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post