
Na Mwandishi Wetu, Kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali ya Tanzania, kupitia Mgodi wake wa Bulyanhulu imeendelea kuboresha mazingira ya elimu ya msingi kwa kuongeza ujenzi wa madarasa katika shule ya mchepuo wa Kingereza ya Kharumwa iliyopo Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoa wa Geita. Shule hii imejengwa kwa fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Mradi wa kuongeza madarasa ulianza Aprili 30, 2025, unatarajiwa kukamilika September 11, 2025.Mwaka huu Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale imepata Sh100,996,200 kwa ajili ya kutekeleza ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa, na kununua samani kwa ajili ya kuondoa changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa.Akizungumza wakati wa kupokea Mwenge wa Uhuru ulioambatana na kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo hivi karibuni, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Bw Ismail Ali Ussi, aliipongeza Kampuni ya Barrick Bulyanhulu kwa kuendelea kuunga mkono jitihaza za Serikali za kuboresha maisha ya wananchi kupitia uwezeshaji wa miradi katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu.“Nachukua fursa hii kuwapongeza wataalamu wote wa Halmashauri na Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha Watanzania wananufaika na miradi mbalimbali inayotekelezwa katika wilaya hii,” alisema Bw Ussi.Hivyo, alitoa wito kwa wananchi wa Wilaya ya Nhang’hwale kuwapeleka watoto waso shuleni. “Hakuna tena kisingizio cha umbali mrefu wa shuleni kwa sababu shule zinajengwa kila sehemu na hii inatokana na ushirikiano wa Serikali na wadau kama Barrick. Hakika Barrick mnazidi kumheshimisha Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,” alisema Bw Ussi.Alifafanua kwamba ushirikiano unatolewa na kampuni ya Barrick kupitia migodi yake hapa nchini kiashiria cha uwekezaji wenye tija kwa taifa na kuwataka wawekezaji wengine kuiga mfano wa kampuni ya Barrick kwa kuchangia miradi ya maendeleo ya wananchi.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale, Mhe Grace Kingalame alisisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii na kuendelea na ari hiyo ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa viwango vya juu ili kukidhi mahitaji ya wananchi.Alisisitiza kwamba kampuni ya Barrick kupitia mgodi wake wa Bulyanhulu wamekuwa wakishirikiana kwa karibu katika miradi yote ya maendeleo kwa maslahi mapana ya Taifa.Mwakilishi wa Barrick katika hafla hiyo, Bw Samson Mashala, ambaye ni Afisa Uhusiano wa Jamii katika Mgodi wa Bulyanhulu, alisema mgodi utaendelea kufanya kazi na Serikali kuhakikisha miradi ya CSR iliyoibuliwa na wananchi inatekelezwa kwa viwango na kuboresha maisha ya wananchi. “Mradi huu utaondoa shangamoto ya mrundikano wa wanafunzi katika darasa moja na kuboresha mazingira ya wanafunzi.”Aliongeza kwamba mradi huo umefikia 85% ya ukamilishaji wake na utaongeza chachu ya wanafunzi kujifunza katika mazingira mazuri na kuchangia matokeo Chanya katika sekta ya elimu hapa nchini. Mradi umetekelezwa kwa mfumo wa force akaunti unatarajia kupunguza tatizo la madarasa, mrundikano wa wanafunzi wengi kwenye madarasa na kuchochea mazingira rafiki ya kujifunza.Mwisho
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Bw Ismail Ali Ussi (kushoto) akifungua uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa madarasa ya shule ya mchepuo wa kiingereza, Wilaya ya Nyang’hwale, Mkoani Geita , kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Hiyo, Grace Kingalame

Post a Comment