" HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YADHAMIRIA KUONDOA ULEMAVU WA KUONA NA KUBORESHA AFYA YA MACHO MKOA WA SONGWE

HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA YADHAMIRIA KUONDOA ULEMAVU WA KUONA NA KUBORESHA AFYA YA MACHO MKOA WA SONGWE

Na mwandishi wetu, Misalaba Media -SongweKatika hatua muhimu ya kupunguza upofu unaepukika, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) na Shirika Helen Keller International leo  wamewasili mkoani Songwe kwaajili ya kutoa Huduma Mkoba ya matibabu ya ugonjwa wa mtoto wa jicho “Cataract Management” kwa wananchi takribani 700 wa Songwe katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi (Vwawa).Akiongea na waandshi wa habari, Dkt. Jofrey Josephat Mratibu wa Huduma za macho Mkoa wa Songwe ameeleza kuwa kambi hiyo ya siku 6 imelenga kukabiliana na magonjwa ya mtoto wa jicho vilevile kusogeza huduma hizo adimu katika maeneo ya karibu na wanapoishi (vijijini) ambapo imekuwa ngumu kupatikana na gharama kwa wananchi kuzifwata katika hospitali kubwa. “Kambi hii ya siku 6 inalenga kupunguza au kuondoka kabisa tatizo la ugonjwa wa mtoto wa jicho Tanzania “Cataract Management” mwananchi wa maeneo ya vijijii ambapo wamekuwa waadhirika wakubwa kutokana na kukosekana kwa huduma hizo na wataalamu waliobobea katika matibabu ya magonjwa ya macho katika maeneo yanayowazunguka na uwepo wa gharama katika kufuata huduma hizo hospitali kubwa zimekuwa ni kikwazo kikubwa kwa waathirika.”Dkt Jofrey ameendelea kusema kuwa viko visababishi ugonjwa wa mtoto wa jicho baadhi ikuhusishwa na umri mrefu, wakati wengine wanahusishwa na mtindo wa maisha au watu wenye kisukari wana uwezekano mkubwa wa kupata mtoto wa jicho mapema maishani, pia matumizi ya muda mrefu ya dawa za steroid pia inaweza kuongeza hatari.Dkt. Barnabas Mshangila, Daktari Bingwa wa Macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, ameeleza kuwa huduma hiyo ya matibabu ya upasuaji ya mtoto jicho inawezesha kurudisha nuru kwa mtu ambaye alikua haoni na kuweza kuiona dunia tena.“upasuaji huu unachukua muda mfupi na magonjwa haezi sikia maumivu kwa sasbabu anapewa dawa ya kuzuia maumivu na baada ya siku moja kufanyiwa upasuaji magonjwa  anaweza kurudia kuona tena: – Dkt. BarnabasNaye Meneja Mradi wa Shirika la Kimataifa la Helen Keller, Athumani Tawakali amesema wanaendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa Huduma za upasuaji mtoto wa jicho kwa wananchi wa Wilaya ya Songwe pia ameshukuru Uongozi Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Mkoa wa Songwe kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakipatiwa na ameeleza kuwa Mradi huu, unaofadhiliwa na Alcon Foundation, unalenga kuboresha huduma za afya ya macho kwa kurejesha kuona kwa maelfu ya wananchi katika mkoa katika mikoa ya Songwe, Mbeya, Njombe na  Iringa.Nao Edward Mkoko na Ericka Mzihowakazi wa mkoa wa songwe waliojitokeza kupata huduma za matibabu hayo, wameishukuru Serikali, Wataalamu wa macho na waandaji wa kambi hiyo kwa kuwasogezea huduma hiyo karibu na maeneo yao bila malipo au gharama nyinginezo.Kama sehemu ya jitihada hizi, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana na Helen Keller Intl, wamejiandaa kuendesha kambi ya siku 6 ya upasuaji wa mtoto wa jicho katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kuanzia tarehe 12 hadi 19 Septemba 2025 ambapo inatarajiwa wananchi zaidi ya 700 wafanyiwa matibabu ya upasuaji wa mtoto wa jicho.



🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 

Post a Comment

Previous Post Next Post