Na Mwandishi Wetu, Misalaba Media -TarimeTimu ya wataalamu wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikali katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI) ilitembelea Mgodi wa Barrick North Mara ambao unaendeshwa kwa ubia na serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals katika juhudi za kutambua mchango wake kwenye maendeleo ya jamii, kiuchumi na kuthathimini utekelezaji wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) na Maudhui ya Ndani (Local content).Timu ya wataalamu hao wa TEITI walifanya ziara hiyo mwishoni mwa wiki wakiongozwa na Mkuu wa Sehemu ya Utafiti , Andrew Eriyo alisema kwamba eneo kubwa linalopewa kipaumbele katika ziara hiyo ni Uwajibikaji kwa Jamii (CSR)na Maudhui ya Ndani (Local Content) na jinsi inavyowanufaisha watanzania na hasa jamii inayozunguka migodi.“Lengo kubwa ni kutathmini utekelezaji wa kanuni za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) na Maudhui ya Ndani (Local Content) ushirikishwaji wa watanzania kwenye sekta ya madini hapa nchini ,” alisema Eriyo.Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko, aliwakaribisha wataalamu hao wa TEITI katika mgodi uliopo kaika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Mkoani Mara. “Karibuni sana, Uwajibikaji kwa Jamii ni suala la msingi, na tathmini kama hizi huwa zinasaidia sana kuboresha mambo kwenda vizuri zaidi na kupiga hatua mbele za kimaendeleo kwa maslahi ya nchini yetu,” alisema Lyambiko. Alisema kwamba Mgodi wa Barrick North Mara unatumia mabilioni ya fedha kugharimia miradi ya maendeleo katika vijiji vya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, huku suala la ‘Muadhui ya Ndani ’ nalo likipewa kipaumbele na kufungua fursa kwa watanzania kupata kazi kwenye migodi.“Tuna miradi ambayo imekamilika na ambayo utekelezaji wake unaendelea , Mfano kuna upanuzi wa mradi wa maji Nyangoto ambao ulitembelewa na Mwenge wa Uhuru hivi karibuni,” alisema Meneja Mahusiano ya Jamii wa Mgodi wa huo, Francis Uhadi.Uhadi alitaja miradi mingine iliyokamilika kuwa ni pamoja na utengenezaji wa madawati zaidi ya 9,000 ambayo yamegawiwa kwenye shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha sekta ya elimu kwa kuboresha mazingira ya ufundishaji na miundombinu.Madawati hayo yamegharimu shilingi milioni 800 za CSR, Uhadi alisema.“Tuna miradi mingine mingi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), ukiwemo ujenzi wa zahanati, vyumba vya wagonjwa wa nje, madarasa na hata uzio katika shule kadhaa hapa Wilayani,” aliongeza Uhadi.Kuhusu suala la ‘Maudhui ya Ndani’, mgodi huo unatoa kipaumbele kwa wazawa kwenye suala la ajira na fursa za kibiashara kwa jamii zinazozunguka mgodi huo unaoendeshwa kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni tanzu ya Twiga Minerals.“Mfano, tumeweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa kazi zisizohitaji stadi zozote wanapewa watu waliopo maeneo jirani na mgodi,” Uhadi alieleza.Ujumbe huo wa TEITI ulitembelea pia miradi mbalimbali inayotekelezwa kwa fedha za Uwajibikaji kwa Jamii ( CSR) na kuliridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na kampuni ya Barrick katika kuchangia maendeleo ya watanzania. “Mgodi wa Barrick North Mara umekuwa ni mdau wetu mkubwa na leo tumewatembelea kuangalia wanavyofanya kwenye eneo la Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) na Maudhui ya Ndani (local content) ,” alisema mmoja wa watalaamu hao kutoka TEITI, Anastazia Ryoba.Mbali na North Mara, Kampuni ya Barrick pia inaendesha Mgodi wa Bulyanhulu uliopo Wilaya ya Kahama, Mkoani Shinyanga.TEITI ni taasisi ya serikali inayohamasisha uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za madini, mafuta na gesi asilia ili kuhakikisha mapato yanayotokana na rasilimali hizo yanakuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya watanzania na Taifa kwa ujumla.Mwisho
Timu ya watalaamu kutoka TEITI ikitembelea baadhi ya miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ikiwemo ya elimu katika vijiji vilivyo jirani na mgodi wa North Mara mwishoni mwa wiki


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment