Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na
Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, amempongeza askari wa Jeshi la Polisi
mkoa wa Shinyanga na msanii wa Hip Hop, Nyumbu Mjanja (CPL Gabriel Kayaga), kwa
kutumia sanaa yake kufikisha ujumbe wa elimu kwa wanafunzi.
Dkt. Gwajima alitoa pongezi hizo kufuatia ubunifu wa
msanii huyo ambaye amekuwa akitumia muziki na maonesho yake kuhamasisha
wanafunzi kuhusu umuhimu wa elimu, maadili na kujitambua.
Alisema matumizi ya sanaa katika kutoa elimu ni njia
yenye ufanisi mkubwa, hasa kwa vijana, kwani huwavutia na kuwafanya kupokea
ujumbe kwa urahisi zaidi.
Nyumbu Mjanja ambaye pia ni askari wa Polisi mkoa wa
Shinyanga, wakati akizungumza na Misalaba Media, amesema ataendelea kutumia
sanaa yake kama chombo cha kuleta mabadiliko chanya katika jamii, hususan kwa
vijana na wanafunzi.
Hatua hiyo imepongezwa na wadau mbalimbali wakieleza
kuwa ushirikiano kati ya viongozi na wasanii unaweza kusaidia kuimarisha utoaji
wa elimu kwa njia bunifu na yenye mvuto kwa kizazi cha sasa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment