Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto,
ametoa maelekezo mbalimbali kwa viongozi na wanachama wa chama hicho
akisisitiza nidhamu, uwajibikaji na kujitegemea kiuchumi, huku akionya kuwa
uongozi usiofanya kazi hautavumiliwa.
Ngoto ametoa maelekezo hayo wakati wa hafla ya
uzinduzi wa shughuli za chama na ukarabati wa ofisi ya kanda iliyofanyika
mkoani Shinyanga, Aprili 26, 2026 ambapo amewataka viongozi wote kuanzia ngazi
ya mkoa, wilaya, kata hadi matawi kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Amesema ni lazima kila kiongozi awajibike katika
nafasi yake na kuhakikisha chama kinaendelea kuwa imara, akisisitiza kuwa wale
watakaoshindwa kuwajibika wataondolewa ili kupisha wengine wenye uwezo.
“Mtu yoyote ambaye hatakuwa anawajibika
hatutamvumilia, tutawaondoa ili kutoa nafasi kwa wengine wanaoweza kusimamia
majukumu yao ipasavyo,” amesema Ngoto.
Aidha, amewataka viongozi wa ngazi ya mkoa kusimamia
viongozi wa wilaya, huku wale wa wilaya wakisimamia kata na matawi ili
kuhakikisha uwajibikaji unazingatiwa katika kila ngazi ya uongozi.
Katika kusisitiza mshikamano wa chama, Ngoto ameeleza
kuwa nidhamu ni msingi muhimu wa mafanikio, akibainisha kuwa chama hakiwezi
kusonga mbele bila kuwepo kwa heshima na ushirikiano miongoni mwa wanachama
wake.
“Nasisitiza suala la nidhamu, kila mmoja
amheshimu mwenzake, chama kisicho na nidhamu hakiwezi kufikia malengo yake,” amesema
Ngoto
Pia ametoa wito kwa wanachama, hususan vijana na
wanawake, kujishughulisha na shughuli za kiuchumi ili kujiepusha na utegemezi
unaoweza kuwafanya kushawishika kirahisi kisiasa.
Amesisitiza kuwa katika uongozi wake hataki kuona
wanachama wasiokuwa na shughuli za kuwaingizia kipato, akiwahimiza kufanya kazi
ndogo ndogo zitakazowawezesha kujitegemea.
“Napenda wanachama wanaofanyakazi, kila
mmoja ahakikishe anatafuta kipato chake, hali ya utegemezi inaweza kudhoofisha
misimamo ya chama,” amesema.
Ngoto pia amewataka wanachama kujiepusha na tamaa za
madaraka, akieleza kuwa baadhi ya waliokuwa viongozi walihama chama wakaahidiwa
nafasi mbalimbali ambazo hadi sasa hawajazipata.
Katika hatua nyingine, ametangaza kuwa chama kina
mpango wa kufanya chaguzi za kujaza nafasi zilizo wazi ndani ya chama, ambapo
amewahimiza wanachama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi hizo pindi tarehe
rasmi itakapotangazwa.
“Tunazo nafasi wazi, chama kina watu bora
kabisa wa kujaza nafasi hizo, hivyo jitokezeni kugombea ili kuendeleza
mapambano ya chama,” amesema Ngoto.
Awali kabla ya hotuba ya mwenyekiti, Katibu wa CHADEMA
Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami, alitoa taarifa fupi akieleza sababu za
kuanza kwa mpango wa ukarabati wa ofisi ya kanda, akibainisha kuwa hatua hiyo
inalenga kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi wa utendaji wa chama.
Amesema ukarabati na upanuzi wa ofisi ya CHADEMA Kanda
ya Serengeti, ni sehemu ya juhudi za kuimarisha miundombinu na shughuli za
chama katika ukanda huo.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka
mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu, ambapo baadhi yao walipata nafasi ya
kuzungumza na kusisitiza umuhimu wa mshikamano ndani ya chama.
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawama, akitoa taarifa fupi kuhusu mpango wa ukarabati wa ofisi ya kanda.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto, akizungumza na viongozi na wanachama wakati wa uzinduzi wa ukarabati wa ofisi ya kanda uliofanyika mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto, akisalimiana na viongozi mbalimbali wa chama mara baada ya kuwasili kwenye hafla ya uzinduzi mkoani Shinyanga.

Afisa mipango na uchaguzi wa CHADEMA kanda ya
Serengeti Bwana Joseph Ndatala akitoa maelezo kwa ufupi kabla ya zoezi la
uzinduzi.

Afisa mipango na uchaguzi wa CHADEMA kanda ya
Serengeti Bwana Joseph Ndatala akitoa maelezo kwa ufupi kabla ya zoezi la
uzinduzi.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto, akizindua rasmi ukarabati wa ofisi ya kanda katika hafla iliyofanyika Shinyanga.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto, akizindua rasmi ukarabati wa ofisi ya kanda katika hafla iliyofanyika Shinyanga.
Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto, akizindua rasmi ukarabati wa ofisi ya kanda katika hafla iliyofanyika Shinyanga.
Afisa mipango na uchaguzi wa CHADEMA kanda ya
Serengeti Bwana Joseph Ndatala akitoa maelezo kwa ufupi baada ya zoezi la
uzinduzi.

Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto akishiriki
uzinduzi wa ukarabati wa ofisi ya kanda mkoani Shinyanga.

Wanachama wa CHADEMA Kanda ya Serengeti wakisikiliza
kwa umakini maelekezo ya viongozi wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukarabati wa
ofisi mkoani Shinyanga.

Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Lucas Ngoto, akitoa maelekezo kwa viongozi na wanachama kuhusu nidhamu, uwajibikaji na mshikamano ndani ya chama.
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami,
akieleza sababu na umuhimu wa kuboresha miundombinu ya ofisi ya chama.

Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami,
akieleza sababu na umuhimu wa kuboresha miundombinu ya ofisi ya chama.

Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami,
akihamasisha wanachama na wadau kuchangia ukarabati wa ofisi ya kanda.

Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami,
akiendelea kuhamasisha wanachama na wadau kuchangia ukarabati wa ofisi ya kanda.
Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Agatha Mamuya akitoa salamu zake.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment