Na Mapuli Kitina Misalaba
Macho na masikio ya mashabiki wa soka leo Juni 18,
2026 yataelekezwa katika Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga, ambapo Ufukunyungu FC na Duara FC zitamenyana katika
mchezo wa nusu fainali unaotarajiwa kuamua timu ya kwanza kufuzu fainali ya
NIACHEKONA CUP 2026.
Timu hizo mbili zimeonyesha kiwango kizuri tangu
kuanza kwa mashindano hayo na leo zinakutana katika mchezo unaotarajiwa kuwa na
ushindani mkubwa huku kila upande ukiwa na ndoto ya kutinga fainali.
Mashabiki wa timu zote mbili wameendelea kutoa kauli
za kujiamini kuelekea mchezo huo, hali inayoongeza hamasa na mvuto wa pambano
hilo ambalo linatarajiwa kuvuta idadi kubwa ya watazamaji.
Wakati huo huo, mchezo wa pili wa nusu fainali
utachezwa kesho, Ijumaa Juni 19, 2026, ambapo Bulige FC itamenyana na Kashishi
FC kusaka tiketi ya pili ya kucheza fainali ya NIACHEKONA CUP 2026.
Mashindano hayo yameandaliwa na Paul Daud Augustino
maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation, yakilenga
kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha mshikamano wa jamii.
Kwa huduma za MC, matangazo na ushereheshaji wa
matukio mbalimbali, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment