" MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AFARIKI DUNIA KWA KUJINYONGA OLD SHINYANGA

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AFARIKI DUNIA KWA KUJINYONGA OLD SHINYANGA


Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne aitwaye Rebecka Boniphace Maganga mwenye umri wa Miaka 17, anayesoma Shule ya Sekondari Old Shinyanga, amefariki dunia kwa tuhuma za kujinyonga ndani ya chumba alichokuwa akiishi.

Tukio hilo limetokea Aprili 27, 2026 majira ya saa saba mchana katika eneo la Old Shinyanga, baada ya mwanafunzi huyo kudaiwa kujinyonga kwa kutumia mkanda wa sketi ya shule.

Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Janeth Magomi amesema jeshi la polisi lilipokea taarifa za tukio hilo kutoka kwa mlezi wa marehemu, Mashala Piter (56), aliyegundua kifo hicho.

Kwa mujibu wa Kamanda Magomi, uchunguzi wa awali unaonesha kuwa tukio hilo linahusishwa na msongo wa mawazo, baada ya mwanafunzi huyo kurudishwa nyumbani na walimu akitakiwa kurejea shuleni akiwa na mzazi kufuatia kutohudhuria masomo kwa muda wa wiki mbili bila taarifa.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Senyenge, Kijiji cha Old Shinyanga, Benjamin Andrew amesema walipokea taarifa za tukio hilo majira ya saa sita mchana na kufika eneo la tukio ambapo walimkuta mwanafunzi huyo tayari amefariki.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Manispaa ya Shinyanga, Bi. Meryester Nyalusanda ametoa wito kwa wazazi na walezi kujenga ukaribu na watoto wao.

Amesema ni muhimu familia kuwa na mawasiliano ya karibu ili kubaini mapema changamoto wanazopitia watoto, badala ya kuchukua hatua kali kabla ya kuelewa tatizo.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga kwa uchunguzi zaidi, huku jeshi la polisi likiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post