Madereva wa Magari Mkoani Shinyanga wamepatiwa elimu ya usalama barabarani kuhusu utii wa Sheria bila shuruti Kwa kulipa tozo zinazotokana na makosa ya usalama barabarani Kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kuzuiwa na kulipa madeni Kwa lazima pindi tozo hizo zinapokuwa zimeongezeka baada ya siku saba kuisha.Akitoa elimu hiyo Askari Polisi wa Kikosi Cha usalama barabarani Mkoa wa Shinyanga Sajenti David Ndimila amewaelimisha madereva hao kuwa faida ya kulipa tozo hizo mapema inarahisisha usimamizi wa Sheria, inasaidia kuepuka usumbufu mara Kwa mara pia kuepuka adhabu Kali zaidiAidha Sajenti Ndimila amewataka wamikiki wa Magari kuwa na tabia ya kukagua Magari yao pindi wanapotoka kuwapa watu wengine ili kujua kama yameandikiwa faini na kuweza kuwajurisha walioandikiwa faini wazilipe Kwa wakati.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment