Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imefuta uteuzi wa mgombea kiti cha urais wa Chama cha ACT-Wazalendo, Luhaga Joelson Mpina, baada ya kukubali pingamizi lililowasilishwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Hamza Saidi Johari.
Kwa mujibu wa taarifa ya INEC, pingamizi hilo limekubaliwa baada ya kikao cha Tume kilichofanyika Septemba 15, 2025, na hivyo jina la Mpina limeondolewa kwenye orodha ya wagombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Tume ilipokea jumla ya mapingamizi manne: matatu Septemba 13 dhidi ya uteuzi wa Mpina na moja Septemba 14 dhidi ya mgombea wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan.
NEC imeeleza kuwa mapingamizi matatu yamekataliwa. Miongoni mwa yaliyotupiliwa mbali ni:
Pingamizi la Almas Hassan Kisabya (NRA) dhidi ya Mpina.
Pingamizi la Kunje Ngombale Mwiru (AAFP) dhidi ya Mpina.
Pingamizi la Mpina dhidi ya uteuzi wa Dk. Samia Suluhu Hassan (CCM).
Hata hivyo, pingamizi la Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mpina ndilo pekee lililokubaliwa, likisababisha ACT-Wazalendo kupoteza mgombea wake wa urais siku chache kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba 29.
Hii ni mara ya Pili kwa Mpina kukumbana na kadhia hiyo, mara ya kwanza ni alipozuiliwa kurejesha fomu kwa ajili ya uteuzi kufuatia pingamizi lililowekwa na Msajili wa Vyama vya siasa.

Post a Comment