" KUTANA NA BI DEBORAH GORDON ALIYEJITOLEA KUWALEA WATOTO WENYE ULEMAVU NA KUWAPA ELIMU BURE

KUTANA NA BI DEBORAH GORDON ALIYEJITOLEA KUWALEA WATOTO WENYE ULEMAVU NA KUWAPA ELIMU BURE

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaMisalaba Media inaamua kufunga safari hadi kituo cha Grepo Day Care Centre kilichopo Soweto karibu na uwanja wa mpira katika Jiji la Mbeya ili kujionea kazi kubwa anayoifanya Bibi huyo kwa moyo mmoja.Bi Deborah anasema kipaumbele chake sio kupata tu fedha bali ni kuwajali watoto wa aina yoyote ili wapate elimu na kutimiza ndoto zao.Akizungumza na mtandao huu, Bi Deborah Gordon ambaye ni Mwalimu Mkuu wa kituo cha Grepo Day Care amesema waliamua kuwa na kituo hicho baada ya kugundua watoto wenye umri mdogo wamekuwa wakizunguka mtaani tu wakati wazazi wao wakiwa katika majukumu ya kutafuta riziki.Mwalimu Deborah ambaye ameonekana kuwa mama bora amesema kuwa kituo hicho kinaona bora kuwapokea watoto wa aina yoyote wakiwemo wenye ulemavu kwani wote ni watoto na wanahitaji kupata elimu ili waweze kutimiza ndoto zao kama watoto wengine.Amesema kituo hicho kwa sasa kina miaka mitatu tangu kianzishwe, ambapo kilianza kikiwa na watoto 6 na kwa sasa ni watoto 60 wanaoanzia umri wa mwaka mmoja na nusu hadi miaka 6."Tumeona tutoe huduma hii kwani baadhi ya wazazi, hasa akina mama, hawana muda wa kukaa na watoto wao, hivyo tunawajibika kuhakikisha watoto hawa wanajua kusoma, kuhesabu na kuandika pamoja na kuongea lugha zote," alisema Bi Gordon.Shule hiyo yenye walimu wanne, kulingana na madarasa hayo, inahakikisha mtoto kufikia kujiunga na darasa la kwanza anakuwa amejua kila kitu, lengo likiwa ni kuondoa na kutokomeza adui ujinga kwa kizazi cha leo.Aidha, amewahimiza wazazi kuhakikisha wanakuwa na muamko wa kupeleka watoto shule na si bora shule, kwani kumekuwa na changamoto kubwa ya wazazi kuwapeleka watoto kupata elimu bila kujua mtoto anajengwa kwa msingi wa aina gani.Amesema kuwa lengo la kituo hicho ni kutengeneza wasomi wakubwa wanaotokea vyuo vikuu, wakiwemo wahandisi na wasomi wengi zaidi.Ameongeza kuwa kituo hicho kimejitolea kulea pia kuhakikisha kinasaidia serikali kutengeneza ajira, kwani wana vijana 6 waliopewa ujira.Hata hivyo, amesema kuwa kwa awamu ijayo, yaani mwaka 2026, wamejiandaa vyema ambapo wanakwenda kuongeza madarasa ili watoto wasisongamane katika madarasa lakini kuhakikisha wana darasa rasmi ambalo ni la zana mbalimbali za kufundishia watoto na zinauzwa kwa wenye vituo vya kulelea."Kila ifikapo siku ya Ijumaa, watoto hawa hukimbia, hucheza mpira  ambapo pia hupewa chakula kilichoandaliwa katika mazingira safi na salama pia kila siku hupatiwa mboga za majani ambazo nalima mwenyewe, hupata pia  matunda pamoja na  kupumzika wanapochoka, kuogeshwa na kupewa huku usafiri ukiwa unapatikana shuleni hapo na watoto ufundishwa kwa vitendo ili kuwaongezea kumbukumbu.Ikumbukwe kuwa Bi Deborah Gordon ni mbobezi katika Lugha zote kutokana na uzoefu wa kazi hiyo alioupata kutokana na kutembelea Nchi mbali mbali hivyo anatamani watoto wengi wapitie mikononi mwake ili ajivunie.Hata hivyo Ili mtoto wako ajiunge na kituo hicho, wasiliana na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kupitia 0754 88 39 39.

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 

Post a Comment

Previous Post Next Post