WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2025 SHULE YA SEKONDARI NDALA WAKISHEREHEKEA
MAHAFARI YA 16 YA KIDATO CHA NNE TANGU KUANZA KWA SHULE HIYO
Wahitimu kidato cha nne mwaka 2025 Shule ya Sekondari
Ndala, Manispaa ya Shinyanga, wameahidi kufanya vizuri katika Mtihani wa Taifa
unaotarajiwa kuanza Novemba 10, 2025.
Ahadi hiyo wameitoa leo Septemba 18, 2025 katika mahafali ya
16 ya kidato cha nne, ambapo walibainisha kuwa mazingira bora ya kujifunzia na
juhudi kubwa za walimu wao yamewajenga ipasavyo kufanikisha ndoto zao za
kitaaluma na maisha ya baadaye.
Mkuu wa shule hiyo, Mwl. Hamisa Boniphace,
aliwashukuru walimu kwa kujitolea na wazazi kwa mshirikiano wao wa karibu,
akisema mshikamano huo ndio chachu ya mafanikio ya wanafunzi hao.
MKUU WA SHULE YA NDALA MWL. HAMISA BONIPHACE
AKISOMA RISALA KWENYE MAHAFARI YA 16 YA KIDATO CHA NNE 2025 KWA MGENI RASMI KATIKA SHULE YA
SEKONDARI NDALA MANISPAA YA SHINYANGA.
Kwa upande wake, Mwl. Richard Makoye, aliyemwakilisha
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, aliwasihi wazazi kuendelea kuwapa
wanafunzi muda na mazingira tulivu ya kujisomea ili kuwawezesha kufanikisha
malengo yao ya kitaaluma.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Mhe. Magreth Baraka
Ezekiel – Mwenyekiti wa Wachimbaji wa Madini Vijana Tanzania na Mkurugenzi
wa Africa Mining Investment Fund – aliwahimiza wanafunzi hao kuendelea
kuzingatia elimu kama msingi wa mafanikio ya mtu binafsi na maendeleo ya taifa.
“Elimu ndiyo dira ya maisha na msingi wa taifa imara.
Endeleeni kuwa na nidhamu, juhudi na kujituma ili muwe chachu ya maendeleo kwa
taifa la kesho,” alisema Mhe. Magreth.
Shule ya Sekondari Ndala imekuwa mfano wa kuigwa kutokana na
mwelekeo chanya wa ufaulu wa wanafunzi wake. Mwaka 2024, shule hiyo ilishika
nafasi ya 3 kati ya shule 21 za serikali katika Manispaa ya Shinyanga kwa
kupata asilimia 95 ya ufaulu, ikilinganishwa na asilimia 90 mwaka
2023.
Mafanikio haya yametoa matumaini makubwa kwamba wanafunzi wa
kidato cha nne mwaka 2025 wataendeleza mwendelezo wa kung’ara kitaaluma na
kuliandikia taifa historia mpya ya ufaulu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment