Kikundi cha Tuinuane kilichopo kata ya Mwamalili
Manispaa ya Shinyanga, kilichoanzishwa mwaka 2019 kimeendelea kuwa chachu ya
maendeleo ya wanachama wake kupitia mshikamano wa kifedha na michezo ya kuweka
na kukopeshana.
Kwa mujibu wa historia ya kikundi hicho, mwanzo
kiliendesha michezo ya michango midogo ambapo kila mwanachama alichangia kiasi
cha shilingi 200, huku kukiwa na hisa ya shilingi 1,000. Hatua hiyo iliwasaidia
kupata fedha za awali kwa ajili ya kugawana na kuwekeza.
Mwaka 2020, kikundi kilipanua wigo kwa kuanzisha
mchezo wa lazima wa shilingi 200 na mchango wa bati moja, hatua iliyopelekea
kufanikisha ununuzi wa bati 420 zenye thamani ya shilingi 5,760,000.
Aidha, kuanzia mwaka 2022 hadi 2023 wanachama
waliendelea kucheza michezo hiyo na kuongeza mchango wa shilingi 500 pamoja na
hisa, hali iliyoimarisha zaidi mfuko wa kikundi. Hadi kufikia mwaka 2023,
kikundi kimeweza kununua bati 849 zenye thamani ya shilingi 15,282,000 na
baskeli 29 zenye thamani ya shilingi 4,930,000 ambazo zimegawanywa kwa
wanachama wote.
Miongoni mwa malengo makuu ya kikundi hicho ni
kujipatia mashine za kusaga na kukoboa ili kuendeleza shughuli za kiuchumi na
kusaidia wanachama kujitegemea zaidi.
Kikundi cha Tuinuane kimekuwa mfano wa kuigwa kwa jamii kwa kuonesha mshikamano wa kifedha na mikakati ya kujiletea maendeleo endelevu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment