" MHE. KINJEKITILE MWIRU: SITACHOKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI WA KILWA KASKAZINI

MHE. KINJEKITILE MWIRU: SITACHOKA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI WA KILWA KASKAZINI


Na Osama Mohamedi chobo, Misalaba Media -Kilwa Mgombea ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Kinjekitile G. Mwiru, ameahidi kushughulikia changamoto za wananchi kwa bidii na uaminifu mkubwa, akisema yupo tayari kujitoa kwa hali na mali ili kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa jimbo hilo.Akizungumza katika uzinduzi rasmi wa kampeni zake uliofanyika katika Kata ya Kipatimu, Wilaya ya Kilwa, Mhe. Mwiru alisema dhamira yake kuu ni kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi katika sekta mbalimbali zinapatiwa suluhisho la kudumu.> "Nimekuja kufanya kazi, siyo kulala. Tutapambana na matatizo ya muda mrefu katika afya, elimu, maji, barabara, kilimo na uvuvi. Tunataka kuona Kilwa Kaskazini inaondokana kabisa na umaskini," alisema kwa msisitizo.Mhe. Mwiru alisema kuwa, endapo wananchi watamchagua kuwa Mbunge wao, atajitahidi kutembelea kila kata, kusikiliza kero za wananchi na kuzifanyia kazi kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wa maendeleo.Aliongeza kuwa ili kufanikisha malengo ya maendeleo kwa haraka, ni muhimu wananchi wakachagua viongozi kutoka CCM kuanzia ngazi ya urais, ubunge hadi madiwani.> "Ifikapo Oktoba 29, tuhakikishe kura zote ni kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Rais, mimi kama Mbunge wenu, na madiwani wote wa CCM. Tukifanya hivi, kazi itakwenda kwa kasi na tutaweza kutatua matatizo yetu kwa ufanisi mkubwa," alisema Mhe. Mwiru.Katika tukio hilo, mgeni rasmi Mhe. Nape Nnauye, ambaye pia ni kiongozi mwandamizi wa CCM, alihimiza wananchi kumuunga mkono Mhe. Kinjekitile, akisisitiza kuwa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi ni muhimu kwa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita.> "Nimekuja kumuunga mkono Kinje kwa sababu tunahitaji watu wa aina yake — watu wa kazi. Tukikusanyana vizuri tutakuwa na nguvu ya kumbana Dkt. Samia aweze kutimiza ahadi kwa wananchi wa Kilwa," alisema Mhe. Nape.Alisisitiza kuwa ni muhimu kuwa na wawakilishi wanaojua kupigania maslahi ya wananchi ndani na nje ya Bunge ili changamoto za wananchi zisikike na kufanyiwa kazi.


 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post