Na Seif Mangwangi, Simanjiro
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Simanjiro, James Ole Millya, ameahidi kuwaunganisha wananchi wa wilaya hiyo na kuhakikisha wanashirikiana na serikali kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili, ikiwemo migogoro ya ardhi.
Millya aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake uliofanyika katika mji wa Orkesument, tukio lililohudhuriwa na wananchi pamoja na makada wa CCM.
Amesema wananchi wa Simanjiro hawana sababu ya kuendelea kuwa maskini ilhali wanamiliki rasilimali nyingi, ikiwemo nguvu kazi na ardhi ya kutosha, na kwamba kinachohitajika ni kiongozi sahihi wa kuwaunganisha na kuongoza juhudi hizo.“Kazi hiyo nitaiifanya kwa nguvu zangu zote endapo mtanipa ridhaa ya kuwa Mbunge wenu, tukashirikiane na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na madiwani wa CCM kuharakisha maendeleo ya Simanjiro,” alisema Millya.
Kwa upande wao, baadhi ya makada wa chama hicho akiwemo Lembris Kitiri na Sendew Laiser, walisema wana imani kubwa na Millya wakimtaja kama kiongozi mwenye uwezo wa kushirikisha wananchi na kuleta maendeleo ya kweli katika Jimbo la Simanjiro.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi mkoa wa Manyara Janes Darabe amewaasa wana Simanjiro kuhakikisha kura za mheshimiwa rais mbunge na madiwani zinapatikana za kishindo pamoja na madiwani
Post a Comment