
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Kinjikitile Mwiru, ameahidi kuhakikisha kuwa barabara ya Tingi hadi Kipatimu inapitika mwaka mzima, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuboresha miundombinu ya eneo hilo.Akizungumza katika mwendelezo wa kampeni zake katika Kata ya Tingi, Mwiru amesema barabara hiyo ni kiungo muhimu kwa shughuli za kiuchumi na kijamii kwa wananchi wa maeneo hayo, hivyo ni lazima iwe ya kudumu na ipitike bila kikwazo hata katika vipindi vya mvua. "Barabara hii ni uti wa mgongo wa maendeleo kwa wananchi wa Tingi na Kipatimu. Ili uchumi wa eneo hili ukue, lazima tuhakikishe barabara inapitika kipindi chote cha mwaka," amesema Mwilu mbele ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza.Aidha, amewahakikishia wananchi kuwa atashirikiana na mamlaka husika kuhakikisha barabara hiyo inaboreshwa na kuwekewa miundombinu imara ili kuchochea maendeleo ya kilimo, biashara na huduma za kijamii.Wananchi waliokuwa katika mkutano huo walipongeza dhamira hiyo, wakisema wamekuwa wakikumbwa na changamoto kubwa za usafiri hasa nyakati za mvua ambapo barabara hiyo huwa haipitiki kabisa, hali inayokwamisha shughuli nyingi za kiuchumi.Mwiru pia aliahidi kusimamia miradi mingine ya maendeleo ikiwemo afya, elimu na maji safi, endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment