" Mshindi wa zawadi kubwa kupitia kampeni ya Kidigitali ya Bank of Africa azawadiwa shilingi milioni 5

Mshindi wa zawadi kubwa kupitia kampeni ya Kidigitali ya Bank of Africa azawadiwa shilingi milioni 5

 Meneja wa Tawi la Bank of Africa Tanzania tawi la  Moshi, Bi. Mpoki Mwanjala akikabidhi hundi ya mfano ya shilingi milioni 5 kwa Bw. Dolvin Olomi, mshindi wa kampeni ya Miamala ni Fursa, baada ya kutangazwa mshindi wa kampeni hiyo katika hafla iliyofanyika katika tawi la Benki hiyo.


 Mteja wa Bank of Africa-Tanzania (BOA),Bw.Dolvin Salvatory Olomi, kutoka Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro,amebahatika  kuibuka mshindi wa jumla wa shilingi milioni 5 kupitia kampeni iliyomalizika iitwayo “Miamala ni Fursa.”

 Kampeni hiyo, iliyoanza Juni hadi Septemba 2025, iliwezesha zaidi ya washindi 60 nchi nzima kujinyakulia  zawadi, huku wateja wakipata zawadi za kila wiki za Shilingi 50,000 kwa kutumia huduma za kidigitali zinazotolewa na Benki. Kampeni ilifikia kilele kwa droo kubwa ya mwisho, ambayo ilitoa zawadi kubwa  ya Shilingi 5 milioni kwa mtumiaji bora wa huduma ya kidijitali—aliyetangazwa rasmi kuwa mshindi mkuu kupitia droo ya bahati nasibu hiyo.

"Kushinda Shilingi milioni 5  kwa kutumia  huduma ya benki kwa njia ya simu kumebadilisha maisha yangu," alisema Bw Olomi, ambaye alitoa shukurani zake za dhati kwa Bank of Africa-Tanzania,  kwa kukuza ushirikishwaji wa kifedha kupitia kampeni za kibunifu na zenye kuleta manufaa kwa wateja wake.

Kampeni ya “Miamala ni Fursa” ilizinduliwa Juni 4, 2025, na ilianzishwa ili kuhimiza utumiaji wa huduma za benki kidijitali kwa kufanya miamala ya kila siku, ikijumuisha uhamishaji wa fedha kutoka benki  kwa matumizi mbalimbali, kufanya malipo ya ankra,kununua   muda wa maongezi au umeme. Kampeni hii ni sehemu ya dhamira pana ya benki ya kuunga mkono  ajenda ya Serikali ya Tanzania ya  matumizi ya huduma za kidijitali na kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma za fedha kwa wote.

Ofisa Mkuu wa Huduma za Kidijitali wa Bank Of Africa-Tanzania ,Lameck Mushi alisema: "Mafanikio ya kampeni ni ishara tosha kwamba Watanzania wako tayari kutumia huduma za kibenki za kidijitali ambazo ni rahisi, zinaweza kufikiwa na ni zenye manufaa. Kupunguza ada ya uhamisho kutoka benki kwa matumizi mbalimbali kwa zaidi ya asilimia 50% na kufanikisha kuongeza matumizi ya huduma za kifedha kwa njia ya simu kufanya miamala, na msisimko wa kushinda zawadi uliongeza zaidi."

Bw Mushi aliongeza: "Iwe unaishi maeneo ya mjini au vijijini, matumizi ya huduma za Kibenki kwa njia ya simu yalimpatia kila mmoja fursa ya   kushinda. Kampeni hii ni uthibitisho kwamba huduma ya benki ya kidijitali inaweza kuwa ya kila mtu."

Benki pia ilihamasisha  wafanyakazi wake  katika matawi mbalimbali nchini  kuelimisha wateja, watumiaji wapya, na kutoa msaada wa kiufundi muda wote wa kampeni.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano , Nandi Mwiyombella alisema kampeni ya "Miamala ni Fursa” ilikuwa zaidi ya kujitangaza. “Tumewawezesha wateja si tu kwa zawadi za pesa taslimu, lakini pia kuwahakikishia pia wateja wetu kuwa huduma zetu za kidijitali ni zenye uhakika na wanaweza kuzitumia bila wasi”.

 Bank of Africa Tanzania inawashukuru washiriki wote na inampongeza mshindi   wa jumla wa zawadi kutoka Moshi, pamoja na washindi wengine wa kila wiki waliozawadiwa  kwa matumizi ya huduma za kidigitali zinazotolewa na benki.

Wakati benki inao mkakati wa kuleta kampeni za kunufaisha wateja siku za mbele,itaendeleza  dhamira yake kuongeza ujumuishaji wananchi katika sekta rasmi za kifedha na kuwezesha wananchi kunufaika na mapinduzi ya teknolojia na ya kidigitali.

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post