Abiria wanaosafiri kwa masafa marefu wametakiwa kujijengea utamaduni wa kutoa taarifa pindi wanapoona madereva wa magari wakiendesha kwa mwendo kasi, ili kuzuia ajali zinazoweza kujitokeza.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga, ASP Zainabu Mangara, alipokuwa akitoa elimu kwa abiria hao ambapo amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua mapema kabla ajali haijatokea.
ASP Mangara amesema kuwa endapo abiria wataonyesha mshikamano na kutoa taarifa za uvunjifu wa sheria za usalama barabarani, itasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa matukio ya ajali za mara kwa mara.
“Ni vyema mkawa na ujasiri wa kutoa taarifa mapema dereva anapokuwa anaendesha kwa mwendo hatarishi, kwani kinga ni bora kuliko tiba,” amesema ASP Mangara.
Aidha, amewataka abiria kuzingatia kanuni za usalama wakati wa safari na kushirikiana na vyombo vya dola katika kuhakikisha usalama wa maisha yao pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment