" RC MALISA AAHIDI USALAMA KWA WASHIRIKI WA MKUTANO WA INJILI MBEYA

RC MALISA AAHIDI USALAMA KWA WASHIRIKI WA MKUTANO WA INJILI MBEYA

Na Lydia Lugakila

Mbeya 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Wakili Beno Malisa amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka kwa Mhubili wa Kimataifa, Pastor Ezekiel Odero wa New Life Church & Prayer Center kutoka nchini Kenya.

Wamekutana Septemba 16, 2025 huku lengo la mkutano huo likiwa ni kusalimiana, kujitambulisha, na kumjulisha Mhe, Malisa juu ya ujio wa Mkutano Mkubwa wa Injili utakaofanyika jijini Mbeya.

Pastor Ezekiel anatarajiwa kufanya Mkutano wa Injili ambao utaanza Septemba 24-28, 2025, katika Viwanja vya Chuo Cha Kilimo Uyole.

Katika mkutano huo, huduma za kiroho zitakazotolewa sambamba na fursa za kiuchumi zitakuwepo, hasa kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kuweza kuuza bidhaa zao, kwani mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na watu wengi kutoka Mbeya na nyanda za juu kusini kwa ujumla.

Mhe. Malisa amewahakikishia usalama wa kutosha kwa kipindi chote watakachokuwepo mkoani Mbeya na amewasisitiza wananchi kujitokeza ili kupata huduma za kiroho na fursa za kiuchumi.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post