" SAJENTI NDIMILA ATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA VIJANA WA CAR WASH SHINYANGA

SAJENTI NDIMILA ATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA VIJANA WA CAR WASH SHINYANGA

Vijana wanaojihusisha na shughuli za uoshaji magari (Car wash) katika Manispaa ya Shinyanga wamepewa elimu ya usalama barabarani ili kuepuka kuendesha magari ya wateja wao bila kuwa na sifa za udereva.

Elimu hiyo imetolewa na Askari Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, ambaye amewataka vijana hao kuacha mara moja vitendo vya kuendesha magari ya wateja kwani vinachangia ajali, uharibifu wa mali na hata vifo.

Amesema baadhi ya waosha magari hujikuta wakiendesha magari hayo bila uzoefu na kushindwa kuyamudu, hali inayosababisha kugonga watu au vitu vilivyopo katika maeneo ya karibu na kusababisha madhara makubwa.

Sajenti Ndimila amesisitiza kuwa ni vyema vijana hao wakabaki kwenye jukumu lao la kuosha magari pekee na kuacha uendeshaji endapo hawana leseni, ili kuhakikisha usalama wao na usalama wa vyombo vya moto vya wateja wao.


 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post