Na Osama Mohamedi chobo, Misalaba Media - kilwa Wakulima 39 wa zao la mwani kutoka Wilaya ya Unguja wamepatiwa mafunzo maalum yaliyofanyika katika mji mdogo wa Kilwa Kivinje, mkoani Lindi. Mafunzo hayo yalilenga kubadilishana ujuzi, maarifa ya kilimo cha mwani, pamoja na taarifa kuhusu masoko na usindikaji wa zao hilo.Mafunzo hayo yaliwakutanisha wakulima kutoka Unguja na Kilwa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kukuza ushirikiano baina ya wakulima wa pande hizo mbili, sambamba na kuongeza tija katika uzalishaji wa zao la mwani ambalo ni miongoni mwa mazao ya kimkakati ya biashara nchini Tanzania.Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Afisa Maendeleo ya Jamii Uchumi, Bi. Joice Denis, alisema kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kutoa fursa kwa wakulima kubadilishana uzoefu, kupata taarifa sahihi kuhusu masoko, na kujifunza mbinu bora za usindikaji na uhifadhi wa mwani.> “Kupitia mafunzo haya, wakulima wataweza kujifunza kutoka kwa wenzao, kujenga mitandao ya kibiashara, na kuongeza maarifa yatakayosaidia kuinua kipato chao,” alisema Bi. Denis.Aidha, aliongeza kuwa mafunzo hayo yatafungua milango ya ushirikiano mpana kati ya wakulima wa Kilwa na Unguja, na kuwajengea uwezo wa kuwa mabalozi wa kilimo cha mwani katika jamii zao pindi watakaporejea.Kwa upande wao, wakulima kutoka Unguja walieleza kuwa wamejifunza mambo mengi mapya kutoka kwa wenzao wa Kilwa, hasa namna mbalimbali za kutumia mwani kwa matumizi tofauti, hali ambayo imewapa motisha ya kuboresha shughuli zao za kilimo na kuongeza kipato.Wawakilishi hao 39 wanatarajiwa kutumia elimu waliyoipata kwa kuwahamasisha na kuwajengea uwezo wakulima wengine katika maeneo yao, huku wakichangia kwa vitendo katika kuboresha kilimo cha mwani nchini Tanzania

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment