Na Lucas Raphael, Misalaba Media - Tabora MGOMBEA wa kiti cha udiwani kwa tiketi yachama cha mapinduzi (CCM),manispaa Tabora Kessy Sharif Abdulrahaman amesema ataitendea haki ilani ya uchaguzi ya mwaka 2025/2030.Hayo aliyasema kwenye uzinduzi wa kampeni za kata hiyo zilizofanyika mtaa wa Liwale manispaa Tabora.Abdulrahaman alisema ataendeleza mema na mazuri ya kimaendeleo ambayo aliyaanzisha na kuyasimamia akishirikiana na halmashauri.Alisema katika awamu iliyopita akiwa diwani wa kata hiyo yako anajivunia kwenye miradi ya maendeleo ambapo alimpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuiletea kata hiyo ya Gongoni fedha jumla ya Tsh Bilioni 1,400,100 zilipokelewa kwa ajili ya miradi ya maendeleo.Abdulrahaman alifafanua kuwa endapo atachaguliwa tena nawananchi ataisimamia ipasavyo ilani ya uchaguzi 2025/2030 kwa kuendeleza miradi yote ama yale yaliyomo kwenye ilani hiyo katika sekta zote zilizoaiinishwa.Alisema moja yaliyopo kwenye ilani ni upande wa elimu ambapo ndani ya miaka mitano iliyopita yaliyofanyika ni ujenzi wa vyumba vya madarasa matano,ujenzi wa matundu ya vyoo na ukarabati wa shule nzima kwa ujumla.Mgombea huyo wa udiwani anabainisha kuwa kwa upande wa ukarabati wa shule hiyo ambayo ina miaka 80 toka kuanzishwa kwake jumla ya Tsh milioni 480 zilipokelewa kwa ukarabati,ujenzi vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo pamoja ubadilishaji wa paa.Akizungumzia zaidi elimu alifafanua kuwa ipo mipango ambayo ameanzisha ni ujenzi wa ama kuongeza vyumba vya madarasa,sambamba na ujenzi wasekondari eneo la shule ambayo itakuwa ya Ghorofa.“Sambamba na hilo katika shule ya sekondari itakayoanzishwa katika maabara yake atapambana kuhakikisha na kupata milioni 60 ili kuweka miundombinu bora kwa ajili ya kufundishia wanafunzi.”alisema.Aidha, Abdulrahaman alisisitiza ndani ya miaka mitano ijayo endapo atachaguliwa tena kwa kushirikiana na Halmashauri kuendeleza kwa kuweka samani ndani ya ofisi ya kata baada ya kupatikana kwani hapo awali walikuwa wamepanga nyumba ya mtu binafsi.“Ndani ya miaka mitano ijayo ntasimamia ujenzi wa barabara zitakazoainishwa,usimamizi upande wa elimu kama ujenzi wa vyumba vya madarasa na ufaulu wa wanafunzi katika shule ya msingi Town School. na sekondari ya kata hiyo Lwanzari”.alisema.Aidha alisema kuwa kwa mwaka 2020/2025 jumla ya Tsh milioni211,270,100 zilitumika kutengeza barabara ambazo ni barabara za mitaa 12,barabara ya JM Hotel,Brabara ya Afya Usagara na Songoro.Mwisho-
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment