" DKT BALOZI BASHIRU AWAASA VIJANA KUEPUKA PROPAGANDA ZA WALIOKOSA UTEUZI

DKT BALOZI BASHIRU AWAASA VIJANA KUEPUKA PROPAGANDA ZA WALIOKOSA UTEUZI

 Na Lucas Raphael, Misalaba Media - Tabora

KATIBU mkuu kiongozi mstaafu balozi Dkt Alli Bashiru amewaasa kundi la vijana mkoani Tabora kuchukua tahadhari za propaganda za wachache ambao baada kukosa nafasi za uteuzi wanatengeneza chuki.

Kauli hiyo aliitoa katika uwanja wa shule ya msingi Kazembe wakati wa uzinduzi wa kampeni za udiwani na ubunge kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora.

Balozi Dkt Bashiru ambaye ni mratibu wa kampeni kanda kwa mikoa ya Tabora,Kigoma na Singida alisema wapo baadhi ya wanaccm ambao wanapokuwa na nafasi mbalimbali ndani ya chama serikali ni wepesi wa kutamka CCM OYEE lakini wanapokosa nafasi katika uteuzi neno hilohuwezi kusikia vinywani mwao zaidi huwa wanatengeneza nongwa na chuki.

Alisema wanaccm tunapaswa kuwa wakweli muda wote bila kujali una cheo au nafasi ndani ya chama na serikali.

Aidha katika hatua nyingine Balozi Dkt Bashiru aligusia kundi la vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kutaka vijana kuelezwa ukweli  na hasa historia ya mkoa wa Tabora kuwa ni kitovu cha uhuru wa nchi hii.

Alisema licha ya Tabora kuwa na chimbuko la uhuru wa nchi ili wasitumbukie linapaswa kuelezwa ukweli kuhusu mazuri yaliyofanywa na serikali ya CCM.

“Nayasema haya kuhusu vijana maana wapo wachache wanaopotosha ukweli kuhusu maendeleo ya nchi hii na kwamba CCM haijafanya chochote katika suala la zima la maendeleo yayofikiwa hadi sasa.”alisema.

Alisema serikaai ya CCM imefanya mengi makubwa ya kimaendeleo katika sekta zote toka uhuru hadi sasa hivyo ni jambo jema la kujipongeza wanaccm na wananchi kwa ujumla.

“Ni kweli kama nchi na viongozi kwa ujumla bado tuna kazi kubwa ya kufanya mengine kwa wananchi wetu licha ya mazuri na mema yaliyofanyika hadi sasa na serikali ya CCM.”alisema.

Kwa upande wake mgombea wa nafasi ya udiwani kwa tiketi ya CCM kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora Gulamhussein Remtullah alisema na kuishukuru CCM kwa kumuona anafaa kwenye nafasi hiyo ya kugombea udiwani.

“Tulikuwa wengi tukiomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo….hivyo chama kimeona nafaa kugombea nafasi hiyo hivyo sina budi kushukuru.”alisema.

Remtullah alifafanua kuwa kwa kupewa nafasi hiyo atashirikiana na viongozi wenzake na halmashauri na wananchi kwa ujumla kuendeleza mazuri yaliopo na yajayo.

Alisema nafasi ya udiwani kwake ana uzoefu mkubwa kwani alikuwa diwani katika vipindi vya miaka 15 na zaidi ni kuwa mstahiki Meya, hivyo hakuna kigeni kwake kuwa mwakilishi wa wananchi na kiuongizi kwenye halmashauri.

Mwisho-

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post