Fisi 17 wameuwawa kwenye kata ya Shigala wilayani Busega mkoani Simiyu huku miongoni mwa wanyama hao wawili wakikutwa alama pajani, shanga shingoni na hereni kwenye sikio.
Fisi hao wameuwawa kwenye oparesheni maalumu iliyofanywa na mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) lengo likiwa kutokomeza wanyama hao katika kata ambao wamekuwa tishio kwenye maisha ya binadamu na mifugo yao.
Oparesheni hiyo inafanyika kwa siku saba kutokana matukio hivi karibuni ya watoto wawili kushambuliwa na wanyama hao kwa nyakati tofauti katika kijiji cha Ihayabuyaga kilichopo kata ya Shigala huku mmoja akiuwawa na mwingine kujeruhiwa.
Post a Comment