Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Mbeya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole, Dkt. Tulia Ackson, leo amepiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura cha Tambukareli, kata ya Itezi Magharibi, mkoani Mbeya.Baada ya kupiga kura, Dkt. Tulia amewahimiza wananchi wote wa Uyole kujitokeza kwa wingi kutimiza haki yao ya kidemokrasia kwa amani na utulivu, akisisitiza umuhimu wa ushiriki wa wananchi katika kuchagua viongozi wanaowataka.Dkt. Tulia amesema uchaguzi ni fursa muhimu kwa kila Mtanzania kuchangia katika mustakabali wa taifa kupitia sanduku la kura.


Post a Comment