📌 *Majiko banifu 5,236 kusambazwa na kuuzwa kwa bei ya ruzuku mkoani Shinyanga* 📌 *Wilaya tatu (3) kunufaika na mradi* 📍 *Shinyanga* Serikali ya Mkoa wa Shinyanga kupitia Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Katibu tawala msaidizi rasilimali watu, Ndugu David Lyamongi leo Februari 03, 2026 imepokea mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku.Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa ya mradi, Mhandisi Mwandamizi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Deusdedit Malulu amesema,Serikali kupitia REA imekuja na mpango wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku ambao utasaidia kupunguza athari za kiafya na mazingira zitokanazo na matumizi ya nishati isiyo salama ya kupikia.Aidha, usambazaji na uuzaji wa majiko haya banifu ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa matumizi ya nishati safi ya kupikia wenye dhima mpaka ifikapo mwaka 2034 zaidi ya asilimia themanini 80% ya watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia.Halikadhalika, katika kufanikisha hilo Wakala wa Nishati Vijijini unatarajia kusambaza na kuuza majiko banifu katika wilaya nne za mkoa wa Shinyanga ambazo ni wilaya Kishapu, Msalala, Shinyanga na Ushetu na kila wilaya kupata majiko banifu 1,309.Aidha, mkataba wa mradi huu ulisainiwa kati ya REA na mtoa huduma Kampuni ya Greenway Grameen Infra Private Limited C/O Ecomama Tanzania Limited na utatekelezwa ndani ya miezi 15 ambapo mtoa huduma atasambaza na kuuza kwa bei ya ruzuku majiko banifu 5,236.Aidha, gharama ya mradi ni zaidi ya TZS Milioni 317 ambapo serikali itatoa ruzuku ya asilimia themanini (80%) sawa na zaidi ya TZS Milioni 253.8 hivyo badala ya jiko kuuzwa kwa bei ya awali ya TZS 60,593.22 litauzwa kwa bei ya ruzuku ya TZS 48,474.58 na mwananchi atachangia TZS 12,118.64 tu.Aidha, ndugu Lyamongi ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza kwa vitendo maono ya Mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mwananchi anakuwa na uwezo wa kutumia na kupata nishati safi na salama ya kupikia yenye ufanisi mkubwa, rahisi na nafuu kupatikana. Mwisho .
Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Katibu tawala msaidizi rasilimali watu, Ndugu David Lyamongi akizungumza.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254













Post a Comment