" VIONGOZI WA SMAUJATA MSALALA WAMWOKOA MTOTO MWENYE MIAKA 2 ISAKA, AFIKISHWA KITUO CHA MALEZI

VIONGOZI WA SMAUJATA MSALALA WAMWOKOA MTOTO MWENYE MIAKA 2 ISAKA, AFIKISHWA KITUO CHA MALEZI

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Nabila Kisendi, kwa kushirikiana na viongozi wa Halmashauri ya Msalala wasamaria wema, wamefanikisha zoezi la kumuokoa mtoto mwenye umri wa miaka miwili aliyekuwa akiishi katika mazingira hatarishi akiwa na mama yake mwenye changamoto ya afya ya akili katika Kijiji cha Isaka Station, Kata ya Isaka, Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama.

Tukio hilo lilianza Aprili 11, 2026 ambapo viongozi wa SMAUJATA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkoa Bi. Nabila Kisendi, Mwenyekiti wa Kata Bi. Sophia Emanuel, Pamoja na Katibu wa Halmashauri ya Msalala, Bi. Nives Nyoni waliinua juhudi za kuokoa familia hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mtoto huyo alikuwa akiishi katika mazingira yasiyo salama, akilala maeneo mbalimbali pamoja na mama yake, jambo lililoibua wasiwasi kwa wananchi na viongozi wa eneo hilo.

Baada ya jitihada za siku kadhaa, Aprili 14 majira ya saa mbili usiku, viongozi hao walifanikiwa kumchukua mtoto huyo kutoka kwa mama yake na kumpeleka kwa Mwenyekiti wa Kitongoji wa eneo hilo, Mahamud Hamad maarufu Tolonto, kwa ajili ya usalama wa muda.

Katika kipindi chote cha zoezi hilo, viongozi wa SMAUJATA walikuwa wakishirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi pamoja na maafisa ustawi wa jamii wa Halmashauri ya Msalala, akiwemo Richard Jackson Ignace Lifulila na Madam Magori.

Baadaye, mtoto huyo alifikishwa katika kituo cha kulelea watoto yatima kilichopo Kagongwa, Wilaya ya Kahama, kwa ajili ya malezi na uangalizi zaidi.

Aidha, ofisi ya ustawi wa jamii ya Msalala ilisaidia gharama za usafiri ili kufanikisha zoezi hilo, huku mawasiliano zaidi yakifanyika na maafisa ustawi hadi kufanikiwa kuwapata ndugu wa mama huyo, ambao walifika na kumchukua kwa ajili ya uangalizi wa kifamilia.

Viongozi wa SMAUJATA wamewashukuru wote walioshiriki katika zoezi hilo, wakiwemo viongozi wa eneo, maafisa ustawi wa jamii, watendaji wa Isaka Station pamoja na wananchi waliochangia fedha na ushirikiano hadi kufanikisha lengo la kumuokoa mtoto huyo.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post