" KISENDI ATOA WITO KWA VIJANA KULINDA AMANI NA KUJENGA TAIFA

KISENDI ATOA WITO KWA VIJANA KULINDA AMANI NA KUJENGA TAIFA

 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga, Nabila Kisendi, ametoa wito kwa wananchi kuendelea kulinda amani na kudumisha mshikamano katika jamii ili kuhakikisha maendeleo yanaendelea kupatikana.

Akizungumza na Misalaba Media, Kisendi amesema kuwa amani ni msingi muhimu wa ustawi wa jamii na kwamba bila utulivu, juhudi za maendeleo haziwezi kufanikiwa.

Amesisitiza umuhimu wa wananchi kushirikiana na viongozi pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa salama, huku akiwataka kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuhatarisha amani.

Kisendi pia amewahimiza vijana kuwa mstari wa mbele katika kulinda amani, akibainisha kuwa wao ndiyo nguvu kazi ya taifa na wanapaswa kutumia nguvu zao katika shughuli za maendeleo badala ya kujiingiza katika migogoro isiyo na tija.

Aidha, amesema SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga itaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa amani, maadili na mshikamano, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kujenga taifa lenye utulivu na maendeleo endelevu.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post