" KIBENDERA: AWESO VIJANA CUP, NYENZO YA KUKUZA VIPAJI NA AJIRA KWA VIJANA

KIBENDERA: AWESO VIJANA CUP, NYENZO YA KUKUZA VIPAJI NA AJIRA KWA VIJANA

NA: MWANDISHI WETU, PANGANI 

Uwepo wa mashindano ya mpira wa miguu ya Aweso Vijana Cup yanayoratibiwa na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wilayani Pangani mkoani Tanga, yameonekana kuwa jukwaa muhimu la vijana katika kukuza vipaji na kupata ajira kupitia sekta ya michezo.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa mashindano hayo, Ramadhani Kibendera, Aprili 20, 2026, wakati alitoa mwelekeo wa mashindano hayo ambayo kwa sasa yapo mzunguko wa pili wa mtoano.

"Vijana wa Pangani wamehamasika haswa kushiriki mashindano haya ya Aweso Vijana Cup. Kwangu nayaona mashindano haya kuwa ni jukwaa la vijana katika kunoa vipaji vyao na kujiweka katika nafasi nzuri ya kujikwamua kiuchumi kwani kwa sasa nchini kwetu, michezo ni miongoni mwa sekta vinazotoa ajira kwa vijana na kubadili hali zao ya kimaisha," amesema Kibendera.

Aidha, Kibendera amesema tangu kuzinduliwa kwa mashindano hayo, timu zimeonyesha nidhamu ya hali ya juu huku michezo yote ikichezwa katika hali ya amani na utukivu.

"Nidhamu ya wachezaji na mabenchi yote la ufundi kwa timu zote zinazoshiriki ligi hii ni nzuri, michezo yote imechezwa katika hali ya utulivu mkubwa kwani sheria zote 17 zinazoongoza mpira wa miguu zinazingatiwa kikamilifu," amesisitiza Kibendera.

Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi Aprili 04, 2026 na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Musa Mwakitinya yakiwa na lengo la kuhimiza umoja na mshikamano miongoni mwa vijana, kukuza vipaji na ajira, huku yakidhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Pangani na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post