Diwani wa Kata ya Itende katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Andambike Mwakyusa, ametaja vipaumbele alivyojiwekea ili kuhakikisha kata hiyo inafikia maendeleo yanayostahili.
Mwakyusa ametoa kauli hiyo wakati akiongea na misalaba media ambapo amesema ataongozwa na sera na ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufanya maendeleo.
Diwani Mwakyusa ameeleza kuwa vipaumbele hivyo vitatekelezwa kulingana na bajeti na taratibu mbalimbali zilizowekwa na Serikali ya CCM, huku pia akibainisha baadhi ya vipaumbele vyake binafsi kulingana na uwezo alionao.
Amesema kuwa Kata ya Itende bado ni changa kimaendeleo, hivyo inahitaji miundombinu ya barabara inayounganisha vijiji, mitaa na vitongoji.
Amepongeza juhudi zilizofanywa, ikiwemo ujenzi wa barabara ya lami inayofika hadi kituo cha bajaji katika mtaa wa Itende Kati yenye urefu wa takribani kilometa mbili.
Hata hivyo, ameongeza kuwa bado kuna kilometa tatu zilizobaki ambazo ziko katika hali mbaya, zikiwa na makorongo na mashimo makubwa, hali inayohitaji uwekaji wa makaravati.
Amesema barabara hizo zinapitika kwa shida, licha ya jitihada za wananchi kufukia mashimo.
Diwani huyo pia amempongeza Meya wa Jiji la Mbeya kwa kazi nzuri wanayoifanya, akisema wameweka mipango madhubuti ya kuhakikisha kila kata inafikiwa na huduma ya barabara.
Ameahidi kuendelea kushirikiana na wananchi kuhakikisha barabara za mitaa zinakarabatiwa kupitia nguvu za wananchi.
Amesema jiji limejipanga vyema kwa kununua mashine ya kushindilia, na tayari ratiba ya kazi hizo imeanza.
Aidha, amesema kuwa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeahidi kuboresha barabara kwa kiwango cha changarawe, huku kiasi cha shilingi milioni 10 kikiwa kimeingizwa kwenye akaunti ya kata ili kuendeleza kazi hizo.
Kuhusu huduma ya maji, diwani huyo amesema bado kuna changamoto ya upatikanaji wa maji ya kutosha licha ya jitihada za mamlaka husika kusambaza huduma hiyo.
Ameeleza kuwa ongezeko la watu na ukame wakati wa kiangazi husababisha upungufu wa maji.
Ameshukuru juhudi za Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini Patrick Mwalunenge kwa kusaidia kuchimba kisima cha maji ili kupunguza tatizo hilo wakati suluhisho la kudumu likisubiriwa kupitia mradi wa Kiwila.
Katika sekta ya biashara, amesema kata hiyo haina soko rasmi, hali inayowalazimu wananchi kusafiri umbali mrefu kupata bidhaa.
Amesema mipango inaendelea ya kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa soko, na mazungumzo na wananchi tayari yameanza.
Kwa upande wa umeme, diwani amesema huduma ipo na imeboreshwa kwa kiasi kikubwa, huku akimshukuru Rais Samia pamoja na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa juhudi kubwa zinazofanyika
Amesisitiza kuwa mahitaji bado ni makubwa, na baadhi ya maeneo yanahitaji kuunganishwa na kuboreshwa nguvu ya umeme ili kuepuka uharibifu wa vifaa.
Mhe Diwani ameongeza kuwa ana matumaini kuwa kwa ushirikiano wa serikali na wananchi, pamoja na usimamizi mzuri wa bajeti, kata ya Itende itaendelea kupiga hatua za maendeleo.
Hata hivyo ameahidi kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu masuala ya migogoro ya ardhi na umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment