Mbunge wa Viti Maalum mstaafu kutoka Mkoa wa
Shinyanga, Salome Makamba, leo Oktoba 29, 2025, mapema asubuhi ametimiza haki
yake ya kikatiba kwa kupiga kura kuchagua viongozi katika nafasi ya Udiwani,
Ubunge na Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamba amepiga kura katika Kituo cha Kupigia Kura
Bugweto, kilichopo Shule ya Msingi Bugweto, Kata ya Ibadakuli, ndani ya Jimbo
la Shinyanga Mjini.
Akizungumza na Misalaba Media baada ya kupiga kura, amesema
amefurahishwa na utulivu uliopo katika kituo hicho na amewahimiza wananchi wote
waliojiandikisha kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya msingi kwa amani na
utulivu.
Amesema kuwa zoezi la kupiga kura ni msingi wa demokrasia, hivyo ni muhimu kila mwananchi kushiriki ili kuchagua viongozi wanaoamini watawaletea maendeleo.












Post a Comment